• HABARI MPYA

  Sunday, April 09, 2023

  SALAH AKOSA PENALTI LIVERPOOL YADROO 2-2 NA ARSENAL


  WENYEJI, Liverpool wamelazimishwa sare ya 2-2 na Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield, Liverpool.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Mohamed Salah dakika ya 42 na Roberto Firmino dakika ya 87, wakati ya Arsenal yamefungwa na Gabriel Martinelli dakika ya nane na Gabriel Jesus dakika ya 28.
  Liverpool ingeweza kuondoka na pointi zote tatu kama Salah angefunga penalti dakika ya 54.
  Kwa matokeo hayo, Arsenal inafikisha pointi 73, ingawa wanaendelea kuongoza Ligi kwa pointi sita zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao, Liverpool wanafikisha pointi 44 katika mchezo wa 29, ingawa wanabaki nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SALAH AKOSA PENALTI LIVERPOOL YADROO 2-2 NA ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top