• HABARI MPYA

  Wednesday, April 05, 2023

  FOUNTAIN GATE YASHINDA 7-1 MICHUANO YA CAF AFRIKA KUSINI


  TIMU ya Fountain Gate Secondary School ya Dodoma imeanza vyema mechi zake za Kundi A michuano ya shule za sekondari ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), upande wa wasichana kwa ushindi wa 7-1 leo dhidi ya wenyeji, Edendale Technical SchoolUwanja wa the King Zwelithini Jijini Durban, Afrika Kusini.
  Mabao ya Fountain Gate yamefungwa na Winfrida Hubert matano na Mary Siyane mawili na sasa timu hiyo itakamilisha mechi zake za kundi hilo kwa kumenyana na Scan Aid ya Gambia.
  Michuano hiyo, maarufu kama African Schools Football Championship iliyoanza leo Uwanja wa the King Zwelithini Jijini Durban itafikia tamati Aprili 8 na Kundi B Wasichana linaundwa na timu za CEG Mfilou ya Kongo, Anse Boileau ya Shelisheli, CEG Colby ya Benin na Ecole Omar IBN Khatab ya Morocco.
  Upande wa wavulana Kundi A kuna Clapham High School (South Africa), CS Horizon of Bukavu (DRC) na CEM Belaouche Mouhend Oulhadji (Algeria), wakati Kundi B kuna Salima Secondary School (Malawi), Complexe Scolaire Ben Sekou Sylla (Guinea), CEG Sainte Rita (Benin) na Royal Giants High School (Uganda).
  Taasisi ya Motsepe Foundation, inayomilikiwa n Rais wa CAF imechangia dola za Kimarekani Milioni 10 kwenye michuano hiyo na kuifanya iwe ya kitajiri Zaidi miongoni mwa michezo ya wanafunzi barani. 
  Mshindi kwa upande wa wasichana na wavulana atazawadiwa USD 300,000 kila mmoja na washindi wa pili watapata USD 200,000 wakati wa tatu atapata USD 150,000.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FOUNTAIN GATE YASHINDA 7-1 MICHUANO YA CAF AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top