• HABARI MPYA

  Wednesday, April 05, 2023

  OKRAH ALIYEKARIBIA KUWALIZA YANGA OKTOBA 23 AREJEA MZIGONI SIMBA


  WINGA wa kimataifa wa Ghana, Augusitne Okrah amerejea mazoezini  wa Simba SC baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na maumivu.
  Anarejea kuelekea mchezo wa Robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ia Ihefu SC Ijumaa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
  Anarejea karibu na mechi ya marudiano ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya watani, Yanga SC Aprili 16 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Ikumbukwe Okrah aliifungia Simba SC bao la kuongoza dakika ya 15 Oktoba 23, mwaka jana ikitoa sare ya 1-1 na Yanga ambao walisawazisha kupitia kwa kiungo wa Kimataifa ya Burkina Faso, Stephane Aziz Ki dk. 45.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OKRAH ALIYEKARIBIA KUWALIZA YANGA OKTOBA 23 AREJEA MZIGONI SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top