• HABARI MPYA

  Monday, September 11, 2017

  DE BOER ATUPIWA VIRAGO CRYSTAL PALACE

  Frank De Boer amefukuzwa Crystal Palace baada ya matokeo mabaya Ligi Kuu ya England PICHA ZAIDI GONGA HAPA  


  HIZI NDIZO MECHI ZILIZOMFUKUZISHA KAZI DE BOER PALACE

  Agosti 12: v Huddersfield (nyumbani) - lost 3-0
  Agosti 19: v Liverpool (ugenini) - lost 1-0
  Agosti 22: v Ipswich Town (LC) - won 2-1 
  Agosti 26: v Swansea (nyumbani) - lost 2-0
  Sept 10: v Burnley (ugenini) - lost 1-0 
  KOCHA Frank de Boer amefukuzwa katika klabu ya Crystal Palace leo na nafasi yake itachukuliwa na Roy Hodgson Uwanja wa Selhurst Park. 
  De Boer anafukuzwa kutokana na matokeo mabaya, baada ya kushindwa kupata japo pointi au kufunga bao moja katika mechi nne za awali za Ligi Kuu ya England, ikiwemo ya Jumapili ambayo walifungwa na Burnley.
  Hodgson anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili The Eagles baada ya kumzidi kocha mwenzake wa zamani wa England, Hodgson na Sam Allardyce waliyekuwa naye sambamba katika kwenye mbio za kuwania nafasi hiyo. 
  Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka The 70 anatarajiwa kurejea kwenye Ligi Kuu ya England kwa mara ya kwanza tangu alipoondoka West Brom kujiunga na timu ya taifa mwaka 2012, baada ya awali kuzifundisha Liverpool, Fulham na Blackburn katika michuano hiyo mikubwa ya klabu nchini humo. 
  Amekuwa nje ya kazi tangu England ivurunde kwenye michuano ya Euro 2016, ilipotolewa na Iceland, lakini mtu huyo kutoka taifa la Croydon anakwenda kufundisha klabu aliyoichezea akiwa kijana mdogo miaka ya 1960.
  Kuondoka kwa De Boer pia kutamfanya na Sammy Lee aondoke klabuni hapo, ambaye aliingia kwenye klabu hiyo pamoja na Allardyce, na Ray Lewington anawasili katika benchi la Ufundi la Hodgson.

  WASIFU WA KOCHA HODGSON 

  1976–1980: Halmstad
  1982: Bristol City
  1982: Oddevold
  1983–1984: Orebro
  1985–1989: Malmö
  1990–1992: Neuchâtel Xamax
  1992–1995: Switzerland
  1995–1997: Inter Milan  
  1997–1998: Blackburn Rovers
  1999: Inter Milan (caretaker) 
  1999–2000: Grasshoppers 
  2000–2001: Copenhagen
  2001: Udinese
  2002–2004: United Arab Emirates
  2004–2005: Viking
  2006–2007: Finland
  2007–2010: Fulham
  2010–2011: Liverpool
  2011–2012: West Bromwich Albion
  2012–2016: England 
  2017: Crystal Palace 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DE BOER ATUPIWA VIRAGO CRYSTAL PALACE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top