• HABARI MPYA

    Saturday, January 08, 2022

    AZAM FC YAIFUATA YANGA KIBABE NUSU FAINALI MAPINDUZI


    TIMU ya Azam FC imekamilisha mechi zake za Kundi A Kombe la Mapinduzi kwa ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya wenyeji, Yosso Boys jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
    Mabao ya Azam FC yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Idris Mbombo mawili dakika ya 40 kwa penalti na 66, beki Mghana Daniel Amoah dakika ya 51, kiungo mzawa, Ismail Aziz Kada dakika ya 57 na Munzil Abdallah aliyejifunga dakika ya 74, wakati bao pekee la Yosso Boys limefungwa na Daudi Francis Hiluka dakika ya 19.
    Kwa ushindi huo, Azam FC inamaliza na pointi tisa kileleni mwa Kundi A, na sasa itamenyana na washindi wa Kundi B na mabingwa watetezi, Yanga katika Nusu Fainali, wakati washindi wa pili wa Kundi A, Namungo FC watacheza na washindi wa Kundi C, Simba SC mechi zote zitachezwa Jumatatu na Fainali itafuatia Alhamisi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAIFUATA YANGA KIBABE NUSU FAINALI MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top