• HABARI MPYA

  Saturday, January 08, 2022

  SIMBA SC YAENDELEZA UBABE KWA YANGA PRINCESS


  MABINGWA watetezi, Simba Queens wameendeleza ubabe kwa watani wao, Yanga Princess baada ya ushindi wa 4-1 leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba Queens yamefungwa na Aisha Djafar dakika ya saba na 82, na Opa Clement dakika ya 54 na 72, wakati bao pekee la Yanga Princess limefungwa na Aisha Masaka kwa penalti dakika ya 76.
  Kwa ushindi huo, Queens wanafikisha pointi 12 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi mbili zaidi ya Fountain Gate Princess wanaofuatia, wakati Yanga wanabaki na pointi zao saba katika nafasi ya sita baada ya timu zote kucheza mechi nne.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAENDELEZA UBABE KWA YANGA PRINCESS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top