• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 02, 2020

  CHILUNDA WA AZAM FC APATA BAHATI NYINGINE, KUJIUNGA NA MOULOUDIA OUJDA YA MOROCCO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Shaaban Iddi Chilunda anatarajiwa kusaini mkataba wa kujiunga na Mouloudia Oujda ya Ligi Kuu ya Morocco.
  Azam FC leo imesema kwamba imefikia makubaliano ya kumuacha mchezaji wake huyo aende Mouloudia D'oujda kukamilisha taratibu za mwisho za kujiunga na miamba hiyo ya soka Morocco.
  Akijiunga na klabu hiyo, Chilunda atakuwa mchezaji wa tatu wa Kitanzania katika ligi ya Morocco baada ya beki wa kushoto, Nickson Kibabage na viungo Simon Msuva wote wanachezea Difaa Hassan El Jadida na Maka Edward wa Moghreb Tetouan.

  Shaaban Iddi Chilunda anatarajiwa kujiunga na Mouloudia Oujda ya Ligi Kuu ya Morocco

  Msuva mwenye umri wa miaka 26 sasa, ndiye aliyefungua mlango wa Watanzania katika Ligi ya Morocco baada ya kujiunga na Difaa El Jadida mwaka 2017 akitokea Yanga ya Dar es Salaam, akafuatiwa na Kibabage kutoka Mtibwa Sugar mwaka jana na Maka aliyetokea Yanga pia mwaka jana.
  Chilunda aliibukia katika tmu ya vijana ya Azam FC mwaka 2012 kabla ya kucheza mechi yake ya kwanza timu ya wakubwa mwaka 2016 na Agosti 7 mwaka 2018 akajiunga na CD Tenerife ya Hispania katika Segunda División (Daraja la Kwanza) kwa mkataba wa miaka miwili.
  Lakini mambo hayakumuendea vizuri huko, akatolewa kwa mkopo kwenda  CD Izarra ya Segunda División B (Daraja la Tatu) kabla ya kurejea Azam FC mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHILUNDA WA AZAM FC APATA BAHATI NYINGINE, KUJIUNGA NA MOULOUDIA OUJDA YA MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top