• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 08, 2020

  GIROUD AMPIKU PLATINI KWA MABAO UFARANSA YAICHAPA 7-1 UKRAINE


  Mshambuliaji Olivier Giroud akishangilia baada ya kuifungia Ufaransa mabao mawili dakika ya 24 na 33 katika ushindi wa 7-1 dhidi ya Ukraine kwenye mchezo wa kirafiki usiku wa jana Uwanja wa Stade de France, Saint-Denis.
  Giroud alikuwa anacheza mechi yake ya 100 kikosi cha Ufaransa jana na amefikisha mabao 42 na kumpiku gwiji, Michel Platini katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa Les Bleus, sasa akizidiwa na Thierry Henry pekee mwenye mabao 51 jumla. 
  Mabao mengine ya Ufaransa yalifungwa na kinda wa miaka 17, Eduardo Camavinga dakika ya tisa, Vitalii Mykolenko aliyejifunga dakika ya 39, Corentin Tolisso dakika ya 65, Kylian Mbappe dakika ya 82 na Antoine Griezmann dakika ya 89, wakati bao pekee la Ukraine lilifungwa na Viktor Tsygankov dakika ya 53 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: GIROUD AMPIKU PLATINI KWA MABAO UFARANSA YAICHAPA 7-1 UKRAINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top