• HABARI MPYA

  Thursday, October 15, 2020

  CHIRWA APIGA MBILI, DUBE MOJA AZAM FC YAENDELEZA UMWAMBA LIGI KUU, YAIPIGA MWADUI 3-0 CHAMAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Mwadui FC mabao 3-0 usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inayomilikiwa na Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake inafikisha pointi 18 baada ya kucheza sita na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tano zaidi ya mabingwa watetezi, Simba na mabingwa wa kihistoria, Yanga ambao hata hivyo wamecheza tano.
  Ushindi wa Azamn FC leo hii umetokana na mabao ya washambuliaji wake wa kigeni, Mzambia Obrey Chirwa aliyefunga mawili dakika za 28 na 63 na Mzimbabwe, Prince Dube dakika ya 61.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHIRWA APIGA MBILI, DUBE MOJA AZAM FC YAENDELEZA UMWAMBA LIGI KUU, YAIPIGA MWADUI 3-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top