• HABARI MPYA

  Alhamisi, Oktoba 22, 2020

  ‘TEACHER’ MUKOKO TONOMBE APIGA BAO PEKEE YANGA SC YAWACHAPA POLISI TANZANIA 1-0 UHURU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA mpya, Mrundi Cedric Kaze ameanza na ushindi mwembamba wa Yanga SC baada ya kuiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza leo na kuichapa 1-0 Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Pongezi zimuendee mfungaji wa bao hilo pekee kipindi cha pili.
  kiungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mukoko Tonombe ambaye hapa Tanzania amepewa jina la utani Teacher, yaani Teacher kutokana na staili yake ya ushangiliaji.
  Tonombo aliye katika msimu wake wa kwanza tu tangu asajiliwe kutoka AS Vita ya nyumbani kwao, Kinshasa amefunga bao hilo dakika ya 70 kwa shuti lilombabatiza beki wa Polisi Tanzania baada ya kupokea pasi ya kiungo Mzanzibari, Feisal Salum.  Na kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 16, sasa ikizidiwa tano na vinara Azam FC ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, wenyeji Tanzania Prisons wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi, Simba SC bao pekee la Samson Mbaraka Mbangula dakika ya 49 akimalizia kazi nzuri ya Michael Ismail Mpesa Uwanja wa Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa. 
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto, Mukoko Tonombe, Tusila Kisinda, Feisal Salum, Yacouba Sogne/Michael Sarpong dk62, Haruna Niyonzima/Ditram Nchimbi dk59 na Farid Mussa/Zawadi Mauya dk77.
  Polisi Tanzania; Peter Manyika, Datius Peter, Juma Hajji, Iddy Mobby, Mohammed Kassim, Pato Ngonyani, Rashid Juma/Hamad Kambangwa dk56, Hassan Maulid, Tariq Seif, Marcel Kaheza/Kassim Haruna dk77 na Pius Buswita. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ‘TEACHER’ MUKOKO TONOMBE APIGA BAO PEKEE YANGA SC YAWACHAPA POLISI TANZANIA 1-0 UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top