• HABARI MPYA

  Monday, October 26, 2020

  SAMATTA ACHEZA KWA DAKIKA 88 FENERBAHCE YAICHAPA TRABZONSPOR 3-1 LIGI KUU YA UTURUKI

  NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana alicheza kwa dakika 88, Fenerbahce ikiibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Trabzonspor Uwanja wa Fenerbahce Sukru Saracoglu Sports Complex Jijini İstanbul.
  Ingawa hakufunga lakini, mshambuliaji huyo wa zamani wa Aston Villa ya England, KRC Genk ya Ubelgiji, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo (DRC), Simba SC na African Lyon za nyumbani, Dar es Salaam alicheza vizuri kabla ya kumpisha Kemal Ademi.
  Trabzonspor walitangulia kwa bao la kujifunga la mshambuliaji Mkongo Benik Afobe dakika ya 23, kabla ya Fenerbahce kuzinduka kwa mabao ya beki Serkan Asan aliyejifunga dakika ya 51, washambuliaji Enner Valencia dakika ya 55 na Papiss Cisse dakika ya 72.


  Ushindi huo unawapeleka Fenerbahçe katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uturuki baada ya kufikisha pointi 14, wakizidiwa pointi mbili na vinara, Alanyaspor kufuatia timu zote kucheza mechi sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA ACHEZA KWA DAKIKA 88 FENERBAHCE YAICHAPA TRABZONSPOR 3-1 LIGI KUU YA UTURUKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top