• HABARI MPYA

  Saturday, October 10, 2020

  MIAMI HEAT YAFUFUA MATUMAINI YA TAJI NBA, YAIPIGA LAKERS 111-108

  TIMU ya Miami Heat imefufua matumaini ya kutwaa taji la Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani baada ya ushindi wa 111-108 dhidi ya Los Angeles Lakers kwenye mchezo wa tano wa fainali ya NBA asubuhi ya leo.
  Sasa timu hizo zitakutana kwa mara nyingine katika mchezo wa sita Jumatatu asubuhi kuamua bingwa wa NBA, ambayo msimu wake ulioanza Oktoba 2019 umechelewa kumalizika kutokana na mlipuko wa virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID 19.
  Kama kawaida LeBron James ameng'ara na kufunga pointi 40 upande wa LA, lakini akafunikwa na Jimmy Butler aliyeifungia Miami pointi 35 ikiwemo mitupo miwili ya pointi tatu tatu.


  LeBron James amefunga pointi 40 LA Lakers ikichapwa 111-108 na Miami Heat, Jimmy Butler akifungia Miami pointi 35 

  Pamoja na kufunga pointi 35, Butler pia alipiga rebounds 12 na assists 11 kwa Miami, wakati James pamoja na pointi 40, pia alipiga rebounds 13 na assists saba upande wa Lakers.
  Ikifanikiwa kushinda Jumapili, Lakers waliongia wamevaa jezi zilizoandikwa 'Black Mamba' kumuenzi gwiji wa timu hiyo, marehemu Kobe Bryant watachukua taji la 17 na kufikia rekodi ya Boston Celtics kutwaa mara nyingi zaidi taji la NBA, kihistoria 17.
  Bryant, na binti yake Gianna, na watu wengine saba walifariki dunia katika ajali ya helikopta Januari 26.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MIAMI HEAT YAFUFUA MATUMAINI YA TAJI NBA, YAIPIGA LAKERS 111-108 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top