• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 18, 2020

  KOCHA KATWILA AJIUNGA NA IHEFU SC SAA CHACHE TU BAADA YA KUACHANA NA MTIBWA SUGAR

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  ALIYEKUWA kocha wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila amejiunga na timu ya Ihefu SC ya Mbarali mkoani Mbeya iliypanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu.
  Katwila, kiungo wa zamani wa Mtibwa Sugar anakwenda Ihefu SC kuchukua nafasi ya Maka Mwalwisi aliyeondolewa wiki moja iliyopita kutokana na matokeo mabaya.
  Hatua hiyo inafuatia saa chache baada ya Katwila kuachia ngazi Mtibwa Sugar, siku moja kabla ya timu hiyo ya Manungu mkoani Morogoro kumenyana na Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kesho.


  Kocha Zubery Katwila amejiunga na Ihefu SC saa chache tu baada ya Katwila kuachia ngazi Mtibwa Sugar 

  Msemaji wa timu hiyo Thobias Kifaru amethibitisha kuondoka kwa kocha huyo na kusema kuwa nafasi yake kwa sasa itashikwa na Kocha msaidizi Vincent Barnabas ambaye atawasimamia wakatamiwa hao hapo kesho.
  “Ni kweli ameuomba uongozi kwamba anahitaji kupumzika, ni kijana wetu tangu akiwa mchezaji” amesema Kifaru huku akiongeza kuwa kwa sasa ni vigumu kuzungumza kuhusu kumwajiri kocha mpya japo amikiri kuwa kwasasa wapo kwenye mchakato.
  Mtibwa Sugar imepoteza mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu, wakianza na Yanga, kisha Biashara United na baadae kwa Gwambina FC.
  Katwila alianza kama mchezaji wa Mtibwa Sugar mwaka 2000 kabla ya kuwa kocha Msaidizi baada ya kustaafu na baadaye kocha Mkuu kwa msimu wa pili sasa.
  Lakini baada ya msimu uliopita timu kunusurika kushuka daraja na mwanzo mbaya msimu huu, amelazimika kwenda kujaribu bahari sehemu nyingine. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KOCHA KATWILA AJIUNGA NA IHEFU SC SAA CHACHE TU BAADA YA KUACHANA NA MTIBWA SUGAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top