• HABARI MPYA

  Jumatatu, Oktoba 12, 2020

  LAKERS YATWAA TAJI LA NBA, LEBRON JAMES AWEKA REKODI MPYA

  TIMU ya Los Angeles Lakers imetwaa ubingwa wa Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani, NBA baada ya ushindi wa pointi 106-93 dhidi ya Miami Heat Alfajiri ya leo kwenye mchezo wa sita wa fainali na kufanya ushindi wa jumla 4-2.
  Hilo linakuwa taji lao la kwanza ndani ya muongo mmoja – mara ya mwisho walibeba taji hilo kwa juhudi za marehemu Kobe Bryant, aliyeshinda taji la tano na la mwisho akiwa na timu hiyo.
  Shujaa wa LA Lakers safari hii ni LeBron James aliyefunga pointi 28, rebounds 14  na assists 10, huku Bam Adebayo akiifungia Miami pointi 25.


  Wachezaji wa Los Angeles Lakers wakipongezana kwa kutwaa ubingwa wa NBA baada ya ushindi wa pointi 106-93 dhidi ya Miami Heat 
  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Hilo linakuwa taji la nne kwa LeBron James, ambaye pia alishinda tuzo ya nne ya Mchezaji Bora (MVP) wa fainali ya NBA – na la kwanza kwake tangu ajiunge na LA mwaka 2018 na ni la kwanza kwa kocha aliye katika mwaka wake wa kwanza, Frank Vogel.  
  Gwiji wa Lakers, Kobe Bryant, binti yake, Gianna na watu wengine saba walifariki kwenye ajali ya helikopta Januari 26.
  Vanessa Bryant, mjane wa marehemu Kobe alifurahia ushindi huo kwa kuposti picha yake akiwa na wakala wake wa zamani, Rob Pelinka, ambaye sasa ni Meneja Mkuu wa Lakers.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LAKERS YATWAA TAJI LA NBA, LEBRON JAMES AWEKA REKODI MPYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top