• HABARI MPYA

    Monday, October 26, 2020

    MTIBWA SUGAR WAICHAPA AZAM FC 1-0 BAO LA KIPINDI CHA PILI LA JAFFAR SALUM KIBAYA GAIRO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BAO pekee la Jaffar Salum Kibaya dakika ya 62 limetosha kuipa Mtibwa Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa CCM Gairo mkoani Morogoro.
    Mtibwa Sugar inafikisha pointi 11 baada ya kucheza mechi nane na kusogea nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakati Azam FC inayobaki na pointi zake 21 baada ya kucheza mechi nane pia – inaendelea kuongoza kwa pointi mbili zaidi ya mabingwa wa kihistoria, Yanga SC ambao hata hivyo wana mchezo mmoja mkononi.
    Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Ruvu Shooting imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi, Simba SC, bao pekee la Nahodha wa Ruvu Shooting, Fully Zulu Maganga dakika ya Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.


    Nayo Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC bao pekee la Ramadhani Ibata dakika ya 88 Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTIBWA SUGAR WAICHAPA AZAM FC 1-0 BAO LA KIPINDI CHA PILI LA JAFFAR SALUM KIBAYA GAIRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top