• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 02, 2020

  TFF YAAHIDI KUYAFANYIA KAZI MALALAMIKO YA YANGA SC JUU YA MKATABA WA SIMBA NA MORRISON

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

  SHIRIKISHO la Soka Tanzana (TFF) limesema limepokea malalamko ya klabu ya Yanga juu ya mapungufu ya mkataba wa winga Mghana, Bernard Morrison na Simba SC na utayafanyia kazi kwa mujibu wa taratibu.

  Yanga SC jana iliwasilisha malalamiko TFF, ikitaka mahasimu wao, Simba wapokwe pointi zote kwenye mechi ambazo Morrison amecheza, kwa sababu mkataba baina yao una mapungufu na haujapitishwa katika mfumo wa usajili (TMS) wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FFA).

  Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Frederick Mwalalebela alidai mkataba huo una sahihi moja tu na kwa ujumla mkataba ambao upo kwenye Mfumo wa Usajili wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kati ya Simba na Morrison umesainiwa na upande mmoja tu, wa mchezaji.


  Yanga imelalamika mkataba wa Bernard Morrison na Simba SC una hitilafu na haujapitishwa FIFA 





  Pamoja na upande wa Simba kutosaini wala kugonga muhuri, pia hakuna tarehe ya kusaini mkataba huo kati ya pande zote mbili husika na hakuna saini za Kamishina wa Viapo na wala mashahidi.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TFF YAAHIDI KUYAFANYIA KAZI MALALAMIKO YA YANGA SC JUU YA MKATABA WA SIMBA NA MORRISON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top