• HABARI MPYA

  Jumatatu, Oktoba 26, 2020

  DEPAY AMTAKIA HERI VAN DIJK BAADA YA KUIFUNGIA LYON


  Mshambuliaji Memphis Depay akishangilia kwa kuonyesha fulana ya kumtakia heri beki wa Liverpool, Mholanzi mwenzake Virgil van Dijk wa Liverpool ambaye ni majeruhi kwa sasa. Depay alifanya hivyo baada ya kuifungia bao la kwanza Lyon dakika ya 12 katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Monaco kwenye mchezo wa Ligue 1 jana Uwanja wa Groupama Jijini Decines-Charpieu. Mabao mengine ya Lyon yalifungwa na K. Toko Ekambi dakika ya 34, H. Aouar kwa penalti dakika ya 41 na K. Toko Ekambi dakika ya 44, wakati bao pekee la Monaco lilifungwa na W. Ben Yedder kwa penalti dakika ya 48
   PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DEPAY AMTAKIA HERI VAN DIJK BAADA YA KUIFUNGIA LYON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top