• HABARI MPYA

  Jumatano, Oktoba 14, 2020

  NEYMAR APIGA HAT TRICK NA KUMPIKU RONALDO KWA MABAO BRAZIL


  Nyota Neymar akishangilia baada ya kuifungia Brazil mabao matatu dakika za 28 na 83 kwa penalti na lingine dakika ya 90 na ushei katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Peru kwenye mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia Amerika Kusini usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Taifa wa Lima, Lima.
  Sasa mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain amefikisha mabao 64 timu yake ya taifa, mawili zaidi ya Ronaldo na 13 nyuma ya Pele, ambaye anaongoza kwa mabao yake 77 kwa mujibu wa hesabu na takwimu za Shirikisho ka Soka la Kimataifa (FIFA).
  Bao lingine la Brazil limefungwa na Richarlison dakika ya 64, wakati mabao ya Peru yamefungwa na André Martín Carrillo dakika ya sita na Renato Fabrizio Tapia dakika ya 59 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NEYMAR APIGA HAT TRICK NA KUMPIKU RONALDO KWA MABAO BRAZIL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top