• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 13, 2020

  YANGA SC WAPATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU, WAICHAPA MBEYA CITY 1-0 KWA MBINDE DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa 1-0 Mbeya City usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijni Dar es Salaam.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee dakika za mwishoni kabisa za mchezo huo, beki wa kati, Mghana Lamine Moro. 
  Yanga SC inafikisha pointi nne baada ya mechi mbili, ikitoka kulazimishwa sare na timu nyingine ya Mbeya, Tanzania Prisons kwenye mechi ya kwanza hapa hapa Dar es Salaam.


  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Omary Mdoe wa Tanga aliyesaidiwa na Abdulaziz Ally wa Arusha na Hamdani Said wa Mtwara, Mbeya City inayofundishwa na beki wa zamani wa Simba SC, Amri Said iliwabana kwa Yanga kwa mchezo wa kujilinda zaidi na kushambulia kwa kushitukiza. 
  Na baada ya kufanya majaribio mengi bila mafanikio kiasi cha kuanza kukata tamaa, hatimaye Moro aliye katika msimu wake wa pili Jangwani akaunganisha kwa kichwa kona maridadi ya kiungo wa kimataifa wa Angola, Carlos Carlinhos dakika ya 86.
  Mechi zilizotangulia leo, Ihefu FC imepata ushindi wa kwanza tangu ipande Ligi Kuu baadd ya kuichapa Ruvu Shooting 1-0, bao pekee la Enock Jiah dakika ya saba Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Nayo Biashara United ikaichapa Mwadui FC 1-0 pia, bao pekee la Deogratius Judika dakika ya 72 Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Metacha Mnata, Kibwana Shomary, Yassin Mustapha, Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto, Mukoko Tonombe, Deus Kaseke/Yocouba Sogne dk46, Feisal Salum/Carlos Carlionhos dk61, Michael Sarpong, Haruna Niyonzima/Ditram Nchimbi dk69 na Tuisila Kisinda.
  Mbeya City; Haroun Mandanda, Kenneth Kunambi, Mpoki Mwakinyuke, Juma Ramadhani, Babilas Chitembe, Abdulrahman Mohamed, Suleiman Ibrahm, Abdul Suleiman, Rashid Mchelenga, Kibu Dennis na Siraj Juma.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC WAPATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU, WAICHAPA MBEYA CITY 1-0 KWA MBINDE DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top