• HABARI MPYA

    Wednesday, October 14, 2020

    KAMATI YA MAADILI YAGOMA KUWASIKILIZA MAWAKILI WA MORRISON, WAMATAKA MWENYEWE AFIKE KWENYE KESI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeshindwa kutoa uamuzi juu ya shitaka la kimaadili linalomuhusu kiungo wa Simba, Bernard Morrison, baada ya mchezaji huyo kutoa udhuru na kushindwa kufika kwenye kamati hiyo kwa madai ya kukabiliwa na majukumu ya klabu yake.
    Mwenyekiti wa kamati hiyo, Wakili Kichere Mwita Waissaka alisema jana kwamba Morrison alituma wawakilishi ambao ni mawakili wake, lakini kutokana na uzito wa shauri lenyewe, kamati inamuhitaji mlalamikiwa mwenyewe badala ya wawakilishi ambao wasingeweza kujibu baadhi ya maswali.
    “Kamati iliona kwamba kuna maswala yanatakiwa kujibiwa na yeye mwenyewe badala ya wawakilishi, kwahiyo suala lake liliahirishwa”, amesema Kichere.


    Morrison anakabiliwa na shtaka la kudharau kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kwa kitendo chake cha kusaini mkataba na Simba wakati shauri lake dhidi ya Yanga kuhusu mkataba wake likiwa bado halijaamuliwa.
    Kuhusu rufaa ya Yanga kwenye Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS), Kichere amesema rufaa hiyo haihusiani na shauri lililopelekewa kwenye kamati hiyo, kwani rufaa ya Yanga inahusu usajili wakati shauri lililo mbele yao linahusu maadili.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAMATI YA MAADILI YAGOMA KUWASIKILIZA MAWAKILI WA MORRISON, WAMATAKA MWENYEWE AFIKE KWENYE KESI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top