• HABARI MPYA

  Jumapili, Oktoba 18, 2020

  SAMATTA ACHEZA HADI MWISHO FENERBAHCE YAWACHAPA WENYEJI, GOZTEPE 3-2 LIGI KUU YA UTURUKI

  Mshambuliaji Mtanzania, Mbwana Ally Samatta (kulia) wa Fenerbahce akimtoka beki wa kimataifa wa Bosnia na Herzegovina wa klabu ya Goztepe SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uturuki leo Uwanja wa Goztepe Gursel Aksel Jijini İzmir. Fenerbahce imeshinda 3-2, mabao yake yakifungwa na José Ernesto Sosa kwa penalti dakika ya 26, Serdar Aziz dakika ya 43 na  Dimitris Pelkas dakika ya 51, wakati ya Goztepe SC yote yamefungwa na Guilherme kwa penalti pia dakika ya 34 na lingine dakika ya 63 akimalizia pasi ya Halil Akbunar. 

  Mbwana Samatta (juu kushoto) aliyecheza hadi filimbi ya mwisho akishangilia na wachezaji wenzake ushindi huo unaowafanya Fenerbahce wafikishe pointi 11 katika mchezo wa tano na kupanda kileleni mwa Ligi, sasa wakiwazidi pointi moja Alanyaspor ambao hata hivyo wamecheza nne


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA ACHEZA HADI MWISHO FENERBAHCE YAWACHAPA WENYEJI, GOZTEPE 3-2 LIGI KUU YA UTURUKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top