• HABARI MPYA

  Ijumaa, Oktoba 09, 2020

  YANGA SC YAICHAPA MWADUI FC 1-0 CHAMAZI BAO PEKEE LA MSHAMBULIAJI MGHANA MICHAEL SARPONG

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imepata ushindi mwembamba katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mwadui FC leo Uwanja wa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Ikicheza kwa mara ya kwanza baada ya kuachana na kocha wake, Mserbia, Zlatko Krmpotic aliyefukuzwa wiki iliyopita baada ya mwezi mmoja tu kazini, Yanga SC ililazimika kusubiri hadi dakika 10 za mwisho kupata ushindi huo.
  Alikuwa ni mshambuliaji Mghana, Michael Sarpong aliye katika msimu wake wa kwanza tangu asajiliwe klabu ya Jangwani aliyefunga bao hilo dakika ya 81 akimalizia kazi nzuri ya kiungo Muangola, Carlos Carlinhos. 

  Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi leo alimuanzisha kiungo majeruhi wa muda mrefu Juma Mahadhi, lakini akampumzisha baada  ya dakika 45 tu.
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Faruk Shikhalo, Kibwana Shomari/Paul Godfrey dk88, Yassin Mustapha, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Said Juma ‘Makapu’, Abdulaziz Makame/Mukoko Tonombe dk46, Juma Mahadhi/Carlos Carlinhos dk46, Deus Kaseke/Zawadi Mauya dk70, Michael Sarpong/Adam Kiondo dk88, Waziri Junior na Farid Mussa.
  Mwadui FC; Mussa Mbisa, Mbarouk Khalfan, Shaaban Kingazi, Abbas Kapombe, Joram Mgeveke, Enrick Nkosi, Wallace Kiango/Salum Chubi dk67, Charles Masenga, Deogratius Anthony, Ismail Ally/Msenga Msenga dk79 na Freddy Cosmas Lewis.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YAICHAPA MWADUI FC 1-0 CHAMAZI BAO PEKEE LA MSHAMBULIAJI MGHANA MICHAEL SARPONG Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top