• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 31, 2020

  YANGA SC YASHINDA MECHI YA SABA MFULULIZO LIGI KUU, YAIPIGA BIASHARA UNITED 1-0 MUSOMA

  Na Mwandishi Wetu, MUSOMA
  VIGOGO, Yanga SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Biashara United jioni ya leo Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.
  Ushindi huo wa saba mfululizo katika mchezo wa nane wa msimu, unaifanya Yanga SC inayofundishwa na kocha Mrundi, Cedric Kaze ifikishe pointi 22, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa wastani wa mabao na Azam FC ambayo hata hivyo imecheza mechi moja zaidi.
  Bao pekee la Yanga SC leo limefungwa na mshambuliaji wake Mghana, Michael Sarpong dakika ya 68 akimalizia krosi ya Ditram Nchimbi kutoka upande wa kulia.


  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, mabingwa watetezi, Simba SC wamezinduka kutoka kwenye vipigo viwili mfululizo baada ya kuichapa Mwadui FC 5-0, mabao ya Nahodha na mshambuliaji, John Bocco na viungo Hassan Dilunga mawili kila mmoja na Said Ndemla moja.
  Namungo FC ikaibika na ushindi wa 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC, bao pekee la Steven Sey dakika ya 66 Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Nao Polisi Tanzania wakaibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons bao pekee la Marcel Kaheza kwa penalti dakika ya 53 Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.
  Kikosi cha Biashara United kilikuwa; Daniel Mgore, Mushta Batozi/Geeshon Samuel dk86, Mpapi Salum, Lenny Kissu, Abdulmajid Mangaro, Hamad Tajiri, Deogratius Judika, Kauswa Bernard, Gerlad Mathias/ Kelvin Friday dk67, Omary Nassor/ Ramadhan Chombo ‘Redondo’ dk46 na Tariq Simba.
  Yanga SC; Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Adeyoum Ahmed, Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto, Mukoko Tonombe, Ditram Nchimbi/ Yacouba Songne dk82, Feisal Salum/ Zawadi Mauya dk88, Michael Sarpong, Waziri Junior/Tuisila Kisinda dk60 na Farid Mussa. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YASHINDA MECHI YA SABA MFULULIZO LIGI KUU, YAIPIGA BIASHARA UNITED 1-0 MUSOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top