• HABARI MPYA

  Jumamosi, Oktoba 03, 2020

  NAMUNGO FC YA MSIMU HUU SI TISHIO, LEO IMEPIGWA TENA NYUMBANI 1-0 NA MWADUI FC

  Na Mwandishi Wetu, RUANGWA
  TIMU ya Namungo FC leo imepoteza mechi ya pili msimu huu nyumbani baada ya kuchapwa 1-0 na Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Bao lililoizamisha Namungo FC leo limefungwa na Ismail Ally dakika ya saba na kwa ujumla huo unakuwa mchezo wa tatu msimu huu Namungo FC inapoteza ndani ya mechi tano.
  Ilianza vyema Ligi Kuu kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union Septemba 6, kabla ya kufungwa 1-0 na Polisi Tanzania hapo hapo Majaliwa Septemba 14 na baadaye ikachapwa 1-0 na Tanzania Prisons Septemba 19 huko Sumbawanga.

  Mechi nyingine ambayo Namungo FC wameshinda ni dhidi ya wenyeji, Mbeya City Septemba 25 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya kabla ya kipigo cha leo.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Mbeya City wamelazimishwa sare ya bila kufungana na ndugu zao, Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu unafuatia Saa 1:00 usiku kati ya vigogo, Yanga SC na Coastal Union ya Tanga Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC YA MSIMU HUU SI TISHIO, LEO IMEPIGWA TENA NYUMBANI 1-0 NA MWADUI FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top