• HABARI MPYA

  Jumatano, Oktoba 21, 2020

  AMRI SAID ATUPIWA VIRAGO MBEYA CITY KUTOKANA NA MWENENDO MBAYA WA TIMU LIGI KUU

  Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Mbeya City imeachana na aliyekuwa kocha wake Mkuu, Amri Said Juma ‘Stam’ kutokana na mwendendo mbaya wa timu katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  Taarifa ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Emanuel Kimbe jana ilisema kwamba  maamuzi hayo yalifikiwa baina ya pande mbili baada ya majadiliano kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu katika ligi kuu inayoendelea.
  Amri Said, beki wa zamani wa Simba SC alijiunga na Mbeya City Desemba mwaka jana ikiwa katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu msimu huu uliopita.


  Lakini timu hiyo ikalazimika kwenda kucheza Play Offs dhidi ya Geita Gold ili kubaki Ligi Kuu na msimu huu hadi sasa inashika mkia kwenye ligi hiyo ikiwa na pointi mbili tu baada ya kucheza mechi saba, ikitoa sare mechi mbili na kufungwa tano.
  Na katika kipindi hiki cha mpito, Mbeya City itakuwa chini ya aliyekuwa Msaidizi wa Amri Saidi, Mathias Wandiba hadi hapo maamuzi mengine yatakapofanyika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AMRI SAID ATUPIWA VIRAGO MBEYA CITY KUTOKANA NA MWENENDO MBAYA WA TIMU LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top