• HABARI MPYA

    Wednesday, January 08, 2020

    AZAM FC YAMSAINISHA MKATABA WA MIAKA MINNE KIUNGO 'FUNDI' WA MLANDEGE, KHLEFFIN HAMDOUN

    Na Mwandshi Wetu, ZANZIBAR
    UONGOZI wa Azam FC, unayofuraha kuwataarifu kuwa tumekamilisha taratibu za kumsajili kiungo mshambuliaji, Khleffin Hamdoun, kwa mkataba wa miaka minne akitokea Mlandege ya Zanzibar.
    Huo unakuwa usajili wa kwanza kwa Azam FC kwenye dirisha dogo la usajili, likiwa ni pendekezo la Kocha Mkuu, Aristica Cioaba.
    Hamdoun, aliyefikisha umri wa miaka 19 leo, amesaini mkataba rasmi wa kuitumikia Azam FC leo Jumatano usiku, mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat'.
    Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat' (kulia) akimkabidhi jezi ya kiungo wa Mlandege ya Zanzibar, Khleffin Hamdoun baada ya kusaini mkataba wa miaka minne leo

    Mara baada ya kusaini mkataba huo, kiungo mshambuliaji huyo alielezea furaha yake ya kukamilisha taratibu ya kujiunga Azam FC huku akiahidi kushirikiana na wachezaji wenzake kuipa mataji timu hiyo.
    Kiungo mshambuliaji huyo alionyesha kiwango kizuri akiwa na timu yake ya Mlandege ilipochuana na Azam FC juzi, jambo ambalo lilimvutia Cioaba na kuidhinisha asajiliwe haraka iwezekanavyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAMSAINISHA MKATABA WA MIAKA MINNE KIUNGO 'FUNDI' WA MLANDEGE, KHLEFFIN HAMDOUN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top