• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 29, 2020

  MTENDAJI MKUU WA AZAM FC AFANYA ZIARA KLABU KADHAA NCHINI MISRI, AKUTANA HADI NA HIMID MAO

  OFISA Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat', akiwa makao makuu ya miamba ya soka barani Afrika, Al Ahly.
  Popat amefanya ziara hiyo leo, kwa lengo kuu la kujifunza mambo mbalimbali ya soka, pamoja na kujionea uwekezaji uliofanywa na klabu hiyo ya karne barani Afrika.
  Aidha kwenye ziara hiyo alikuwa sambamba na mwenyeji wake, Amgad Alghoniny, ambaye ni Mhariri wa kitengo cha habari cha timu hiyo.
  Mbali ya kutembelea kwa miamba hiyo, Popat pia alipata fursa ya kukutana na Nahodha wa zamani wa Azam FC, Himid Mao 'Ninja', anayekipiga nchini humo katika timu ya ENPPI. 
  Hapa akiwa na kiungo wa zamani wa Azam FC, Mtanzania Himid Mao ambaye kwa sasa anachezea ENPPI 
  Hapa akiwa na Himid Mao na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Fiston Abdul Razak anayecheza naye ENPPI 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTENDAJI MKUU WA AZAM FC AFANYA ZIARA KLABU KADHAA NCHINI MISRI, AKUTANA HADI NA HIMID MAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top