• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 17, 2020

  YANGA SC YAFUNGA USAJILI DIRISHA DOGO KWA KUMSAINISHA WINGA MZAMBIA, ERICK KABAMBA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Yanga SC imemsajili mchezaji mpya kutoka Zambia, winga Erick Kabamba kutoka klabu ya Buildcon FC ya kwao, Zambia.
  Mchezaji huyo aliyekuwa anacheza klabu hiyo ya Zambia pamoja na beki Mghana aliyejiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu, Lamine Moro anafanya jumla ya wachezaji wapya waliosajiliwa dirisha dogo kufika saba. 
  Wengine ni viungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima, Mghana Bernard Morrison na mshambuliaji Muivory Coast, Yikpe Gnamien Gislain kwa upande wa wageni ni wazawa, beki Adeyoum Ahmed na washambuliaji Tariq Seif Kiakala na Ditram Adrian Nchimbi. 
  Baada ya kusajiliwa wachezaji hao wapya saba, Yanga imewaacha wengine sita ambao ni Mrundi Suleiman Mustapha, Mnyarwanda Issa Bigirimana Mnambia, Sadney Urikhob, Mzambia Maybin Kalengo, Mganda Juma Balinya na mzawa Muharami Issa ‘Marcelo’.
  Wengine wametolewa kwa mkopo ambao ni mabeki Cleophas Sospeter, Ali Hamad Ali na kiungo Raphael Daudi Lothi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YAFUNGA USAJILI DIRISHA DOGO KWA KUMSAINISHA WINGA MZAMBIA, ERICK KABAMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top