• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 14, 2020

  BARCA YAMFUKUZA VALVERDE, YAMCHUKUA QUIQUE SETIEN

  KLABU ya Barcelona imemteua Quique Setien aliyewahi kutakiwa na Watford kuwa kocha wake mpya baada ya kumfukuza Ernesto Valverde.
  Hii ni mara ya kwanza klabu hiyo inafukuza kocha katikati ya msimu ndani ya miaka 17 na wanafanya hivyo licha ya Barcelona kuwa kileleni mwa La Liga kwa sasa. 
  Kocha huyo mwenye umri wa miaka 61 aliwahi kuhusishwa na kuhamia Watford mwanzoni mwa Desemba kabla hawajamchukua Nigel Pearson.

  Kocha wa zamani wa Real Betis, Quique Setien amesaini mkataba wa hadi mwaka 2022 Barcelona 


  VALVERDE AT BARCA 

  Kujiunga: Mei, 2017
  Mataji: La Liga (2017-18, 2018-19), Kombe la Mfalme (2017-18), 
  Super Cup ya Hispania (2018) 
  Mechi: 145
  Ameshinda: 97
  Sare: 32
  Amefungwa: 16 
  Katika taarifa ya klabu, Barcelona wamesema wanataka kumshukuru hadharani Valverde kwa kutekeleza majukumu yake vyema kitaaluma, lakini kushinda mataji mawili tu ya Hispania imechukuliwa kama matokeo mabaya.
  Alizomewa na mashabiki wa Barcelona nchini Saudi Arabia kwenye mchezo wa Nusu Fainali ya Super Cup ya Hispana wakifungwa na Atletico Madrid Alhamisi iliyopita.
  Baada ya matokeo hayo, klabu ikaamua kumuondoa kocha huyo mwenye umri wa miaka 55 na kumchukua Setien baada ya kukataliwa na Xavi.

  Ernesto Valverde akiondoka viwanja vya mazoezi vya Barcelona, Joan Gamper jana mchana

  WASIFU WA KOCHA MPYA BARCELONA

  Jina: Quique Setien
  Kuzaliwa: Santander, Hispania, Septemba 27 1958 (Miaka 61)
  Klabu alizofundisha: Racing Santander, Poli Ejido, Equatorial Guinea, Logrones, Lugo, Las Palmas, Real Betis 
  Mafanikio: Nafasi ya sita La Liga akiwa na Real Betis (2017-18)  
  Mauricio Pochettino anakubalika mno mbele ya Rais wa klabu, Josep Bartomeu lakini hakutaka kibarua hicho na amewahi kunukuliwa akisema bora akawe mkulima kuliko kufundisha wapinzani wa klabu yake ya zamani, Espanyol.
  Ajabu ni kwamba Setien atapewa mkataba wa kumalizia msimu huu tu na miaka mingine miwili.
  Setien alizaliwa Septemba 27, mwaka 1958 mjini Santander nchini Hispania.
  Na amezifundsha kwa mafanikio makubwa klabu za Racing Santander, Poli Ejido, Equatorial Guinea, Logrones, Lugo, Las Palmas na Real Betis awali. 
  Mafanikio yake makubwa zaidi ni kumaliza katika nafas ya sta kwenye La Liga akiwa na klabu ya Real Betis msimu wa  2017-2018.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BARCA YAMFUKUZA VALVERDE, YAMCHUKUA QUIQUE SETIEN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top