• HABARI MPYA

  Jumamosi, Januari 25, 2020

  MTIBWA SUGAR NA RUVU SHOOTING ZANG’OLEWA KWA MATUTA NA TIMU ZA ‘MCHANGANI’ MICHUANO YA ASFC

  Na Mwandishi Wetu, GAIRO
  MABINGWA wa zamani wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mtibwa Sugar wametupwa nje ya michuano hiyo maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuchapwa kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya 1-1 Uwanja wa CCM Gairo mkoani Morogoro.
  Awadh Salum alitangulia kuifungia Mtibwa Sugar dakika ya 64 kabla ya Hussein Amir kuisawazshia Sahare All Stars ya Tanga dakika ya 83 na kwenye mikwaju ya penalti safari ya mabingwa wa mwaka 2018 wa ASFC ikaishia hatua ya 32 Bora.
  Ruvu Shooting ya Pwani imekuwa timu nyingine ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kuaga mashindano hayo baada ya kuchapwa na Gwambina FC kwa penalti 7-6 kufuatia sare ya 1-1 Uwanja wa Gwambina, Misungwi.

  Mechi nyingne za leo, Alliance imewatoa wenyeji African Sports kwa kuwachapa 1-0 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga, Ndanda SC ikashinda 1-0 dhidi ya Dodoma FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara, Ihefu FC ikaipiga 1-0 Gipco FC na JKT Tanzania ikailaza Tukuyu Stars 2-0 Uwanja wa Uhuru.
  Alliance FC, Ndanda SC, Ihefu FC, JKT Tanzania, Simba SC, Gwambina FC na Sahare All Stars zinaungana na KMC, Panama na Mbeya City kuingia raundi ya tano ya michuano hiyo ambayo bingwa wake hucheza michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  Hatua ya 32 Bora itaendelea kesho kwa vigogo wengine, Yanga SC kumenyana na Tanzania Prisons ya Mbeya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Lipuli na Kitayosa FC Uwanja wa Samora Jijini Iringa na Kagera Sugar dhidi ya Mighty Elephant Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
  Mabingwa watetezi, Azam FC watahitimisha hatua ya 32 Bora kwa kumenyana na Friends Rangers Jumatatu Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR NA RUVU SHOOTING ZANG’OLEWA KWA MATUTA NA TIMU ZA ‘MCHANGANI’ MICHUANO YA ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top