• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 13, 2020

  KMC YAMPA MKATABA WA MWAKA MMOJA NA NUSU KOCHA MRUNDI ALIYEKUWA LIPULI FC

  Na Mwandshi Wetu, DAR ES SALAAM
  UONGOZI wa KMC FC umeingia mkataba wa mwaka mmoja na nusu na kocha Mrundi, Haruna Harerimana baada ya kukidhi vigezo tulivyoweka.
  Harerimana anachukua nafasi ya kocha Jackson Mayanja kutoka Uganda ambaye mkataba wake ulisitishwa kutokana na  timu kutokuwa na mwenendo mzuri katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara na mashindano ya Kimataifa.
  Harerimana amepitishwa na Bodi ya timu ambayo ilipitia maombi mengi ya makocha wa ndani na nje ya nchi.
  Zoezi la kutafuta kocha halikuwa rahisi kutokana na ujuzi na uzoefu wa makocha waliomba kuchukua nafasi ya Mayanja ambapo baada ya kuondoka, nafasi hiyo ilikuwa chini ya kaimu kocha mkuu, Hamadi Ally.

  Kocha Harerimana ametambulishwa kwa wachezaji na tayari ameanza kazi ya kuinoa timu ya KMC kwa ajili ya mashindano ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Azam Sports.
  Uongozi wa KMC unaimani kubwa na Harerimana ambaye awali alikuwa anaifundisha timu ya Lipuli ya Iringa inayoshiriki Ligi Kuu pia.
   “Ni kocha ambaye amekidhi vigezo vyote ambavyo tumeweka na uongozi kuamua kuingia naye mkataba.  Kupitia yeye, tunaamini timu itafanya vyema na kurejesha ubora wake wa msimu  uliopita,” alisema Mwenyekiti wa Bodi ya timu ya KMC, Meya Benjamin Sitta.
  Mechi ya kwanza ya Harerimana itakuwa mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Uhuru na katika mchezo wa kombe la Azam Sports dhidi ya Pan African ambayo pia itachezwa kwenye uwanja wa Uhuru Januari 24.
  Kwa upande wake, Harerimana alisema kuwa amekuja kufanya kazi na kama ilivyo makocha wengi duniani, mafanio ndiyo malengo makuu.
  Alisema kuwa anahitaji wachezaji ambao wanajituma na wenye malengo ya kuleta mafanikio kwa timu na vile vile katika kipaji chake.
   “Nimekuja kufanya kazi yenye mafanikio, hivyo naomba wachezaji tushirikiane katika kuleta matokeo chanya ya timu na kumaliza ligi katika nafasi nzuri. Nimefurahi kupata uongozi ambao unajali maslahi ya wachezaji na watendaji wa timu,” alisema Harerimana.
  Wakati huo huo, Uongozi wa timu ya KMC umefikai makubaliano ya  kusitisha mikataba na wachezaji watano kutokana na sababu mbalimbali.
  Wachezaji hao ni Aaron Lulambo, George Sangija, Rehani Kibingu, Melly Mongolare na Janvier Besala Bokongu. Pia mchezaji Vitalis Mayanga ameuzwa kwa timu ya Ndanda FC ya Mtwara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KMC YAMPA MKATABA WA MWAKA MMOJA NA NUSU KOCHA MRUNDI ALIYEKUWA LIPULI FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top