• HABARI MPYA

    Tuesday, January 28, 2020

    SIMBA SC YAKANA TUHUMA ZA KUTAKA KUMHONGA KIPA WA YANGA, RAMADHANI KAWBILI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Simba SC imesema imeyapokea kwa masikitiko makubwa maelezo ya kipa wa Yanga SC, Ramadhani Awamu Kabwili kuishutumu klabu hiyo kutaka kumhonga aihujumu klabu yake.
    Taarifa ya Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Masingiza leo imesema kwamba kauli za aina hiyo kutoka kwa wachezaji ni za kuchukiza na siyo za heshima ambazo zinaashiria upangaji wa matokeo ya mechi kama ilivyotuhumiwa na mchezaji huyo na klabu yake inazipinga na kukemea vikali.
    “Kauli hizi zina madhara makubwa kwenye uadilifu wa klabu ya Simba na viongozi wake. Uadlifu na heshima Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania kwa ujumla unawekwa mashakani kama kauli za namna hii hizi hazitachukuliwa hatua stahiki,”amesema Senzo katika taarifa yake.
    Hata hivyo, Ofisa huyo Raia wa Afrika Kusini amesema kwamba wamefurahishwa mno na hatua iliyochukuliwa na TFF baada ya kauli za mlinda mlango huyo chipukizi wa kimataifa wa Tanzania.
    Jana TFF iliiagiza Kamati yake ya Maadili kufuatilia ukweli kuhusu tuhuma za upangaji matokeo zilizotolewa na Kabwili kipa aliyedakia timu zote za vijana kuanzia U17 na U20 kabla ya kupandishwa ya wakubwa.
    Kipa wa tatu wa Yanga, Kabwili alinukuliwa na kituo kimoja cha Redio nchini akiishutumu klabu ya Simba kutaka kumpa hongo kwa ajili ya kufanikisha mpango wa kupanga matokeo.
    Alidai Simba ilimshawishi afanye kosa kwenye mechi dhidi ya JKT Tanzania litakalomfanya aonyeshwe kad ya njano na kufikisha idadi ya kadi zitakazomsababisha akose mechi iliyofuata baina ya watani wa jadi katika soka ya Tanzania.
    Hata hivyo, Kabwili aliyesimama langoni kwenye mechi dhidi ya Simba SC Februari 16, mwaka jana, Yanga ikichaowa 1-0, bao pekee la mshambuliaji Mnyarwanda, Meddie Kagere dakika ya 72 amesema hakukubali kushiriki mpango huo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAKANA TUHUMA ZA KUTAKA KUMHONGA KIPA WA YANGA, RAMADHANI KAWBILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top