• HABARI MPYA

    Sunday, January 26, 2020

    YANGA SC YAIPIGA TANZANIA PRISONS 2-0 NA KUTINGA 16 BORA AZAM SPORTS FEDERATION CUP

    Na Asha Said, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Yanga SC imeungana na vigogo wenzao, Simba SC kutinga hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Kwa ushindi huo, Yanga SC watamenyana na Gwambina FC ya Daraja la Kwanza ambayo jana iliitoa Ruvu Shooting kwa penalti 7-6 baada ya sare ya 1-1 Uwanja wa Gwambina, Misungwi.
    Katika mchezo wa leo Yanga SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji, Luc Eymael kwa ushirikiano na gwiji wa klabu, mzawa Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ wakisaidiwa na Riedoh Berdien kutoka Afrika Kusini ambaye ni kocha wa mazoezi ya utimamu wa mwili na Manyika Peter, kocha wa makipa ilipata bao moja kila kipindi.





    Alianza kiungo mpya Mghana, Bernard Morrison kufunga bao la kwanza dakika ya tisa kwa penalti baada ya beki Michael Ismail wa Tanzania Prisons kuunawa mpira kwenye boksi katika harakati za kuokoa krosi ya Balama Mapinduzi.Akafuatia mchezaji mwingine mpya, mshambuliaji Yikpe Gislain Gnamien kutoka Ivory Coast aliyefunga bao la pili kwa kichwa dakika ya 64 kwa kichwa akimalizika pasi ya kiufundi ya Bernard Morrison. 
    Mechi nyingine za leo, Lipuli FC imekuwa timu nyingine ya Ligi Kuu kutolewa baada ya Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting kufuatia kufungwa kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 2-2 na Kitayosa Uwanja wa Samora mjini Iringa.
    Nayo Namungo FC imeifunga Biashara United 2-1, Kagera Sugar imeifunga Mighty Elephant 2-0 Stand United imesonga mbele kwa ushindi wa penalti 5-4 baada ya sare ya 1-1 na Maji Maji FC Uwanja wa Maji Maji mjini Songea.
    Kitayosa, Namungo FC, Kagera Sugar, Stand United  na Yanga SC zinaungana na Alliance FC, Ndanda SC, Ihefu FC, JKT Tanzania, Simba SC, Gwambina FC na Sahare All Stars, KMC, Panama na Mbeya City kuingia raundi ya tano ya michuano hiyo ambayo bingwa wake hucheza michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
    Hatua ya 32 Bora itahitimishwa kesho kwa mabingwa watetezi, Azam FC kumenyana na Friends Rangers Dar es Salaam.
    Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Metacha Mnata, Juma Abdul, Jaffar Mohamed, Lamine Moro, Said Juma ‘Makapu’, Abdulaziz Makame, Deus Kaseke/Patrick Sibomana dk82, Haruna Niyonzima, David Molinga/Yikpe Gislain dk57, Mapinduzi Balama na Bernard Morrison/ Feisal Salum dk98.
    Tanzania Prisons: Jeremiah Kisubi, Michael Ismail, Benjamin Asukile, Vedastus Mwihambi, Nurdin Chona, Adilly Buha, Salum Kimenya/Samson Mbangula d68, Ezekia Mwashilindi, Jeremiah Juma/ Hamid Mohammed dk89, Paul Peter na Aziz Ismail/Cleophace Mkandala dk80.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC YAIPIGA TANZANIA PRISONS 2-0 NA KUTINGA 16 BORA AZAM SPORTS FEDERATION CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top