• HABARI MPYA

    Saturday, January 11, 2020

    JINSI YANGA INAVYOHITAJI KIUNGO MKABAJI KAMA MGHANA JAMES KOTEI

    Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM
    KUMEKUWA na taarifa zinazo muhusisha kiungo wa klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini James KOTEI kujiunga na klabu ya Yanga.
    Ikumbukwe Kotei kabla ya kujiunga na Kaizer Chiefs aliwahi kuitumikia klabu ya Simba ya Tanzania kwa mafanikio makubwa sana!👏👏
    Sasa hebu tuangalia namna ambavyo Kotei anaweza kuleta tija kwa klabu ya Yanga kwa kuangalia  majukumu yake uwanjani.
    Kwenye modern football/au mpira wa kisasa eneo la ulinzi huwa tuna aina 3 za viungo wa chini/typical defensive midfielder,deep lying playing midfielder  na holding midfielder

    Hizi hapa chini ni aina za hao viungo:>👇👇
    👉🏽 Holding midfielder unaweza kusema ni kiungo mkabaji asilia ambaye anakuwa karibu kabisa na walinzi wa timu yake na wakati timu yake inakwenda kushambulia yeye ubakia katika eneo la nyuma ili kuzuia uwezekano wowote wa timu yake kushambuliwa.mfano wa viungo wa namna hii ni Casemiro,Sergio Busquets na Frankie de Jong.
    👉🏽Deep-lying midfielder huyu ni kiungo ambaye anakuwa na ujuzi mkubwa wa kuuchezea mpira na wakati mwingi anawaza kutoa pasi na kupokea uku akili yake ikiwaza kuona mpira unakwenda mbele kwa maana ya kushambulia,uwaza zaidi kushambulia kuliko kuzuia,mfano wake ni Toni Kroos,Thiago Alcantara,na Marco Verratti.
    👉🏽Typical defensive midfielder ni kiungo mahususi kwa ajili ya ulinzi ,mbali na kuwalinda walinzi wake bali uhusika katika kuvunja mashambulizi ya timu pinzani,mfano ya wake ni kama Nemanja Matic,Javier Mascherano,na Ngolo Kante
    👉🏽Unaweza kuona ni aina ambayo zinataka kufanana kwa maana ya uchezaji na kuna baadhi ya wachezaji wanauwezo wa kucheza staili zote kulingana na mpizani wanae kutana nae na mahitaji ya kimfumo walio  ingia nao wachezaji kama Sergio Busquets,Frenkie de Jong na Jorginho wanaweza kutumia kulingana na mahitaji ya timu katika aina zote tatu hapo juu.
    🙌🙌Mfumo wa kiuchezaji  wa Yanga unahitaji mtu aina ya Kotei kwa maana ya typical defensive midfielder/kiungo halisi wa ukabaji) yeye hana habari nyingine zaidi ya kupora mipira na kucheza physical battle watoto wa mjini wanaita kazi chafu kwa maana ya kuvuruga mipango ya timu pinzani katika eneo hilo.
    Kukosekana kwa mtu aina ya Kotei ndiko kumepelekea Yanga kulazimisha kuwatumia wakina Mohamed Issa Banka,Feisal Salum pia kumtumia Papy Tshishimbi kama   deep lying playmaker midfielder ndio maana Feisal  Salum akiwekwa kiungo wa juu anapiga kazi na utaona anakuwa huru sana na kujiamini tofauti akicheza kiungo wa chini ambapo ujaribu kutumia nguvu na kumsababishia kucheza rafu nyingi sana.🙆‍♂🙆‍♂
    Huku pia Papy Tshishimbi na Mohamed Banka wanakuwa kwenye umbo zuri la timu endapo watacheza namba nane,au wakitokea pembeni hii yote kutokana na tabia zao za kuchezea mpira wakati mwingi na kupenda kupress  jambo ambalo linakuwa na tija kwa timu zaidi.👏🏽👏🏽
    Hivyo ukiangalia kwa viungo waliopo sasa Yanga si aghalabu kusema Yanga  inamuhitaji mtu kama KOTEI ili kuja kumaliza tatizo hilo huku akihusika kuwapunguzia kazi walinzi wa kati kwani kazi zote ngumu atazimaliza yeye pale kati huku akitoa nafasi ya walinzi wa kati kukabiliana na mikimbio ya washambuliaji wa timu pinzani ambao kimsingi wanategemea ubora wa sehemu ya kati ya kiwanja..
    Ndio maana  huko nyuma Yanga ilikuwa na watu kama Juma Seif Kijiko,Godfrey Bonny,Mbuyu Twite,Athumani Iddy Chuji,wakati wakiwa kwenye ubora wao tuliona namna ambavyo safu ya ulinzi ilikuwa solid na pia kutoa nafasi kwa viungo washambuliaji kufikiria zaidi kushambulia kuliko kuzuia hivyo kuja kwa kotei kama itafanikiwa itakuwa bora na itatoa uhuru kwa kina Feisal ,Banka kucheza maeneno yao halisi.👍🏽👍🏽
    Kwa maneno mengine klabu ya Yanga ikifanikiwa kuinasa saini ya kiungo huyo itakuwa imeongeza kitu kwenye kikosi jambo litakalo pelekea kutoa matokeo chanya kwenye eneo la ulinzi na ushambuliaji pia.Ni swala la muda tu ila na kuona ni kipi wana Jangwani watakivuna katika hili.👏👏

    (Dominick Salamba ni mchambuzi wa soka anapatikana pia kupitia katika Akaunti yake ya Instagram kama @dominicksalamba na Twitter kama @Dominicksalamb1)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JINSI YANGA INAVYOHITAJI KIUNGO MKABAJI KAMA MGHANA JAMES KOTEI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top