• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 10, 2020

  ATLETICO YAIFUATA REAL MADRID FAINALI KOMBE LA MFALME

  Angel Correa akipongezwa na Koke baada ya kuifungia Atletico Madrid bao la ushindi dakika ya 86 ikiilaza 3-2 Barcelona katika Nusu Fainali ya Kombe la Mfalme jana Uwanja wa King Abdullah Sports City Jijini Jeddah. Mabao mengine ya Atletico Madrid yalifungwa na Koke dakika ya 46 na Alvaro Morata kwa penalti dakika ya 81, wakati ya Barcelona yalifungwa na Lionel Messi dakika ya 51 na Antoine Griezmann dakika ya 62. Atletico sasa itamenyana na mahasimu wao wa Jiji, Real Madrid katika fainali Jumapili hapo hapo King Abdullah Sports City, Jeddah 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ATLETICO YAIFUATA REAL MADRID FAINALI KOMBE LA MFALME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top