• HABARI MPYA

    Wednesday, January 08, 2020

    COASTAL UNION YAICHAPA KAGERA SUGAR 1-0 TANGA NA KUPANDA HADI NAFASI YA PILI LIGI KUU

    Na Mwandishi Wetu, TANGA
    BAO pekee la mshambulaji Ayoub Lyanga dakika ya 77 limetosha kuipa Coastal Union ushindi wa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
    Kwa ushindi huo, Coastal Union inayofundishwa na mchezaji wake wa zamani, Juma Mgunda inafikisha pointi 29 katika mchezo wa 16 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya pili, nyuma ya mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 35 za mechi 14, wakati Azam FC sasa ni ya tatu kwa pointi zake 26 za mechi 13.
    JKT Tanzania wamepata ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Alliance FC Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza, bao pekee la Edson Katanga. Nayo Namungo FC ikapata ushindi wa ugenini wa 3-2 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
    Mechi nyingine tatu za Ligi Kuu leo, zimemalizika kwa sare ya 1-1 KMC na Lipuli Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,  Polisi Tanzania na Biashara United Uwanja wa Ushirika mjini Moshi na Mwadui FC dhidi ya Ruvu Shooting.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COASTAL UNION YAICHAPA KAGERA SUGAR 1-0 TANGA NA KUPANDA HADI NAFASI YA PILI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mwakasege Blog
    Scroll to Top