• HABARI MPYA

    Wednesday, January 15, 2020

    NDOTO YA MAPINDUZI SIMBA SC NA KUMBUKUMBU ZA PATRICK AUSSEMS

    Na Mustafa Mtupa, DAR ES SALAAM
    IKIWA Joto la ubongo wangu limezidi kupanda hata kinywa changu kikawa kina sumbuka kwa kupiga miayo.Akili yangu ikanambia kuwa ulikuwa ni muda sahihi sana wa kupumzisha uti wangu wa mgongo ulio sumbuka siku nzima kutafuta tonge.
    Kiuvivu nikajitupa kitandani na haikuchukua hata dakika tatu tayari nilishaKuwa kwenye kiseto cha usingizi mzito,nikiwa katika kiseto hicho cha haja nikajikuta naamia kwenye ulimwengu wa kifikra,ulimwengu wa ndoto zilizokuwa za  kutisha wakati naziota.
    Nikiwa katika ulimwengu huo wa ndoto za kutisha.nilisafirishwa kifikra na kupitishwa kwenye maji ya kina kirefu cha Bahari hadi nilipofika eneo ambalo nilihisi harufu adhiimu ya marashi ya karafuu hata ikanifanya nigundue kuwa hapo nilipo ni kwenye dimba la Amaan kisiwani Zanzibar ambapo nilikuta Mchezo wa kihistoria wa fainali ya Michuano pendwa kabisa kwenye Jamuhuri hii ya  muungano wa Tanzania.
    Mchezo ambao ulishuhudia ukiwaacha watu wote wakibaki na mshangao ulio ambatana na mshtuko wa kile kilicho kuwa kinatokea kwenye mchezo huo,nikiwa hapo kwenye jukwaa la waandishi wa habari.Sauti  yenye vugu vugu lililo ashiria usadiki wa moja ya maandiko yangu ikapenya vyema kwenye sikio langu la upande wa kushoto na baada ya kumuangalia mwenye sauti hiyo moyo wangu ukalipuka kwa furaha baada ya kumshuhudia muandishi na mtangazaji mkongwe hapa nchini Mahmood Bin Zubery kuwa ndiye aliye ongea maneno yale.Alinambiaa "Mustafa lile andiko lako la kumuaga patrick bado linaendelea kuishi na yale maneno yanaonekana sasa"
    Baada ya kunambia maneni hayoo binafsi nikijikuta nawaza na kuishia kutabasamu kwa tabasamu hafifu kwani nilikuwa nakumbuka ile makala niliyowahi kuandika wakati ule.Na pia nilijikuta nacheka kabisa baada ya kukumbuka baadhi ya waandishi walio ungana kunipinga baada ya kuandika makala hiyo.
    Nilipowaza sababu za kuondoka kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa wana msimbazi hao 'Nkwabi',akili yangu ikanambia kuwa nisi sahau kukumbuka sababu za kuondoka Patrick.
    Nikiwa katika msongo huo wa mawazo taswira ya kumbu kumbu ya 'Tweet' ya Patrick wakati anaondoka ikanijia  na kunifanya nianze kupata mwanga wa kile nilichokuwa nakiwaza .na akili yangu vizuri zaidi baada ya mmoja ya waandishi alipo ning'ata sikio kuwa zile billion 20 bado hazijaiingia kwenye Account ya simba ingawa kuna kiongozi amesema  kuwa mzigo tayari ushasoma.
    Bado maneno ya Patrick ya kusema kuwa kuna viongozi kwenye klabu hii  wataifanya simba izidi kuchelewa kuelekea njia yao ya mafanikio kwakuwa baadhi ya viongozi  wana mawazo mgando bado  inaendelea kuishi.
    Huenda hatukulitazama hili alilo ongea Patrick kwakuwa tuliamini kuwa ilikuwa ni mihemko yake tu kwakuwa amevunjiwa mkataba lakini   naimani kuwa kuna baadhi ya watu wameanza kuelewa kauli zile zilizo semwa nyakati ambazo hakuna aliyetaka hata kuzijadili.
    Siku moja bomu lililo walipua Nkwabi na Aussehms litataka kushuka pia kwa mwengine ili kulinda minong'ono na kuwafanya mashabiki waende Bunju complex kwa furaha.
    Taswira ya kivuli changu inanivuta shati na kunambia kuna mengi ya kuota lakini na kuhoji lakini majibu yake ni adimu  kama  Mbwa kuingia msikitini.
    Ghafla ndoto ya pili inanitawala kichwani na kufanya nipate mshangao wa shauku baada ya kuona chapisho la kwanza la Billionea kijana MO kwenye mtandao wa kijamii wa twitter likijieleza kuwa billionea huyo ametangaza kustaafu na wala haikuchuku hata masaa kadhaa nikashuhudia tena  Billionea huyo akiandika tena kupitia mtandao huo huo kuwa ametangaza kurudi madarakani.nikiwa nimebaki mdomo wazi huku nisijue hata kama nipo Tanzania au Haiti shabiki mmoja wa simba akaropoka kwa kusema kuwa anahitajika kutoa maelezo ya kina juu ya uwekezaji wetu kwenye klabu yetu.haiwezekani mambo yakawa hayaeleweki kama anatukopesha ama anawekeza maana hiyo billioni nne ni za kwetu kwenye zile billioni ishirinu alizonunua Hisa hivyo yeye hawezi kusema eti amelipa wachezaji mishahara wakati ela ni za kwetu wenyewe nayeye amewekeza tu.
    Nikiwa makini kumsikiliza shabiki huyo ghafla alam ya simu yangu ikalia na kunifanya nishtuke kutoka kwenye usingizi ule mzito ulionipeleka kwenye ndoto iliyobeba ukubwa wa maana ya taswira ya Bahari kama utaamua kuitafsiri.nilikaa kitako na kungundua kuwa nina safari ya kuelekea Bandarini kumpokea Katwila na wapiganaji wake nilitabasamu na kujisemea mwenyewe kuwa.Hii ni ndoto ya Mapinduzi yenye kumbu kumbu za Patrick aussehms.

    (Mwandishi wa makala hii, Mustafa Mtupa 'Mtoto wa Mkulima' anapatikana kwa namna 0687058966 na unaweza kumfollow Instageram @Mustafa.mtupa)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NDOTO YA MAPINDUZI SIMBA SC NA KUMBUKUMBU ZA PATRICK AUSSEMS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top