• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 31, 2020

  MIGUU YA MABEKI WA SIMBA SC INAVYOWAHUKUMU MAKIPA WAO

  Na Mustafa Mtupa, DAR ES SALAAM
  ILIKUWA ni mchana ambao uliambatana na hali ya jua kali lililo mchoma yeyote aliyetembea barabarani kwa miguu.
  Nikiwa miongoni mwa watembea kwa miguu hao na kukubali ngozi yangu kushambuliwa na jua kisawa sawa hata vitobo vidogo vilivyo patikana kwenye ngozi yangu vikaruhusu maji yaliyo changanyika na chumvi kutoka kwenye ngozi yangu na kunipa kibaria cha kujifuta kila mara.
  Safari yangu ilikuwa ni kuelekea kwenye moja ya jengo maarufu linalo milikiwa na klabu kongwe hapa nchini na barani Afrika kiujumla kati kati kabisa ya jiji la dar es salaam maeneo ya Karikakoo ambapo ndipo linapopatikana jengo hilo la Klabu ya simba.
  Kwa hakika nilifika japo hali ya miguu yangu ilikuwa haitamaniki kwa kukoga vumbi la kutosha. lakini wala haikuni shughulisha nilisogea karibu kabisa na sehemu niliyoona kuwa kuna watu wameketi na kupiga soga mbali mbali ambazo moja kwa moja niligundua zilikuwa ni soga zinazohusu hali ya kiwango ya timu yao ya Simba.
  Baada ya kufika tu mahala hapo.nikagundua kuwa mada iliyokuwa imesimamisha kijiwe hicho kwa mda wote huo ilikuwa ni kuhusu eneo la golikipa kwenye timu yao huku kuna wengine wakionekana kuamini kuwa Manula ni bora kuliko Beno kakolanya na kuna wengine wanaamini kuwa Beno ni bora kuliko manula.
  Nilijaribu kufikiri kwa kipindi cha zipatazo kama dakika kumi kabla sijamuomba mzee mmoja aliyekuwa pembeni yangu kalamu na nikatoa karatasi na kuanza kuandika barua ambayo baadae niliwaachia wazee hao.
  Barua hiyo ilibeba maudhui yafuatayo.
  Kwa kipindi cha muda kidogo Klabu yenu haijapata kuwa na kipa bora.mmekuwa na makipa ambao wana viwango vya kawaida tu,japo mulionekana kuwa wagumu katika swala zima la kuruhusu nyavu zenu kutikisika.
  Manula aliyeishi Azam hakuwahi tena kufufuka na kuleta maajabu aliyofanya akiwa na wana lamba lamba hao.
  Kitu pekee kilichokuwa kinamuokoa Manula ni kwa sababu alikuwa anapata nafasi ya kucheza tu.binafsi Hakuwa anaonesha kiwango ambacho kingemfanya mvaaji wa jezi kupokea pasi badala ya simu wakati ananyosha nguo.
  Beno kakolanya nae licha ya kuwa alikuwa hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara lakini hata sasa ambapo amepata  nafasi ya kucheza ni kama anaonekana kuwa amesahau namna alivyokuwa anafunga gloves zake alipokuwa anajiangusha kwenye ardhi ya mitaa ya jangwani na kumfanya zahera aoneshe meno yake kwenye sare ya kukumbukwa dhidi ya simba.
  Licha ya ukweli kuwa viwango vya makipa wenu vilikuwa ni vya kawaida saana.lakini bado ukakamavu wa miguu na uimara wa kiakili wa wachezaji wanaounda safu yenu ya ulinzi inayoongozwa na wakongwe Erasto nyoni na Sergie Wawa uliwasahaulisha na kuziba ukweli huu  na kuwaaminisha  kuwa milingoti yenu mitatu inalindwa na mikono salama kabisa.
  Ni wakati huu ambapo Nyoni anaonekana kuwa akili yake imeanza kuchoka na lugha yake ya mwili ikionesha kuwa Akili inataka lakini mwili unakataa.wakati ambao Nyoni anafanya makosa aliyowahi kuyafanya wakati anakomaa.
  Huenda ikawa haya ni matokeo ya mafanikio waliyopata msimu uliopita kwenye michano ya Ndani na nje.😁
  Pia ni wakati huu ambao Pascal wawa anaonekana kuwa anahitaji kuongezewa mafuta kwenye Tanki lake la ubongo.kwani naye anaonekana kuungana na Erasto nyoni kwenye kushindwa kujibu maswali ya kugawanya wakati wameshafika  hadi chuo kikuu huku wakiwa wanasoma uhandisi.
  Udhaifu wa zimbwe kwenye eneo lake pia unachangia kwa kiasi kikubwa ufanyaji wa makosa wa mabeki hawa wawili wazoefu kwani zimbwe anaonekana kukimbia zaidi eneo lake na kuwafanya wakongwe hawa wafanye kazi ambazo waliwahi kuzifanya misimu miwili nyuma ambapo kwa sasa kwao imekuwa ni ngumu kufanya kazi hizo.
  Kapombe sina shida naye ila kama hawa mabeki watatu woote wanafanya makosa kapombe hata akicheza vizuri atawezaje kukaba kwenye eneo lote la ulinzi?
  Aina ya magoli ya mbali ambayo simba wanafungwa wala hamuna haja ya kumtafuta mchawi kwani mulijiroga pale mlipo muacha kotei aondoke na kwasasa matokeo yake ndiyo yale yanaonekana kwani eneo ambalo magoli haya yanafungwa ilikuwa ni majukumua ya kotei ambayo alikuwa anafanya kwa ufanisi wa asilimia %99
  Kwa kumalizia tu ni kwamba mwalimu wangu Mwalimu Kashasha kuna siku aliwahi kunambia kuwa "KIPA BORA NI YULE ANAYEDAKA MIPIRA AMBAYO HATUKUWA TUNA TEGEMEA KAMA ANAWEZA KUDAKA"
  Hivyo kama manula na Beno ni bora,basi inabidi waoneshe ubora wao wakati huu ambao wanapata majaribio ya kutosha.
  Nikahitimisha hivyo barua yangu na kumkabidhi mmoja ya wazee hao.na wala sikutaka kukaa tena eneo hilo nikajongea zangu stendi ya dala dala kugombania magari ya kwetu mbagala.

  Kalamu nyeusi.  Insta.Mustafa.Mtupa. 0687058966
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MIGUU YA MABEKI WA SIMBA SC INAVYOWAHUKUMU MAKIPA WAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top