• HABARI MPYA

    Thursday, January 09, 2020

    AMBAVYO AKILI ZA NIYONZIMA TOFAUTI NA MIGUU YA AJIBU!

    Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM
    KUNA kisa kimoja kidogo nilikipenda sana.Siku moja nilikuwa kijiweni na wana mara paap akapita binti mmoja mrembo sana kila kitu kilisimama kwa muda si unajua tena wanaume na hawa wenzetu ni kama mbwa na chatu.Tulitulia kwa muda tukiheshimu upitaji wake hadi alipomalizikia ,ndipo jamaa mmoja alisikika akisema daaah jaman kuna watu hawana bahati.Wote tuligeuka kulikuoni tena.Jamaa aliendelea huyu dada aliyepita alikuwa ameolewa na jamaa yangu mmoja sasa akiwa kwenye ndoa kuna jamaa akawa anampenda huyu dada wakati akijua tayari ni mke wa mtu muda haukupita yule dada aliachika kwa sababu ambazo sisi hadi leo hatujui,kuona vile jamaa naye akaacha mkewake ili aweze kumuoa yule dada siku anaenda kupeleka barua ya posa anakuta dada anafunga ndoa na jamaa mwingine😳😳😳 unajua nini kilitokea???😂😂😂Siku  nyingine turudi kwenye mada yetu wadauu!
    Misimu miwili nyuma mafundi hawa wa mpira kwa maana ya Haruna Niyonzima na Ibrahim Ajib walikuwa wakitumikia vilabu hivihivi wanavyovitumikia sasa.
    Niyonzima alikuwa Yanga na Ajib alikuwa Simba,baada ya msimu kumalizika ghafla tukasikia Ajib kasajiliwa Yanga,Simba waliumia sana kuondokewa na mchezaji wao kipenzi waliyemlea wenyewe na kumtambulisha katika ulimwengu wa soka na  mbaya zaidi kaenda kukipiga kwa maasimu wao  Yanga,siku zikapita tambo za usajili zikiendelea ghafla Simba yenye jeuri ya fedha za MO ikatikisha vyombo vya habari kwa kuinasa saini ya Haruna Akizimana Fadhili Ally Niyonzima,Ikawa ni kama wasemavyo waswahili kuwa raha ya kuimba ni kupokezana machungu yakahamia kwa Yanga mpaka wakafikia kuchoma jezi za kiungo huyo fundi maestro.
    Msimu ulianza huku Ajib akionekana kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga,akawa mchezaji tegemeo hasa na kukabidhiwa unahodha.
    Kwa upande wa Haruna hali ilikuwa tofauti na matarajio,majeraha yalimuandama,alichelewa kukaa sawa lakini alipokaa sawa alidhibitisha kwa nini amezaliwa Gisenyi pale Rwanda.
    Gisenyi ni eneo lenye watu wenye vipaji vikubwa mno vya soka,wenyewe wanapaita Brazil ya Rwanda.
    Haruna ni mchezaji mwenye matumizi makubwa ya akili,na hiyo ndio silaha yake kubwa,kuna wakati anaweza kukuudhi ukiwa jukwaani kwa pasi zake anazopiga pembeni mwa uwanja na kuzifuata,lakini hiyo imekuwa staili yake kubwa anapokutana na mabeki wagumu kupenyeka,na akifanikiwa kuwafungua kinachofuata ni kucheka tu majukwaani,ukirejea goli lililoipeleka simba robo faina ya #CAFCL dhidi AS Vita Club pale Taifa utakubaliana na mimi,Vita walimchukia sana Haruna usiku ule.
    Ajib ni miongoni mwa wachezaji wenye miguu ya maajabu sana,anaweza kuupiga mpira kivyovyote na ukawa na madhara makubwa mno,wakati mwingine unaweza kudhani labda hayupo kabisa uwanjani kutokana na staili yake ya uchezaji,ila unaweza kujua uwepo wake unapotokea mpira uliokufa,anajua sana huyu mtu,ana mahesabu makali na pasi zenye macho zinazoweza kusafiri umbali umrefu na kufika kwa muhusika pasipo na shaka.
    Unapokuwa mtazamaji na mpenzi wa soka kuna wakati unapata hisia tofauti sana,unaweza kutamani mchezaji fulani ajiunge na timu uipendayo,mimi nipo tofauti kidogo,natamani sana itokee siku miguu ya Ajib ifanye kazi ya pamoja na akili za Haruna Niyonzima,natamani sana niwaone wakicheza timu moja,sio timu moja tu bali kikosi kimoja lakini cha kusangaza bado  wanaendelea kupishana, baada ya Ajib kuwa na uhakika wa kurudi Simba ukawa ndio mwisho wa Niyonzima pale Simba.
    Naamini wanatoa huduma tofauti kabisa,na ndiyo maana Ajib akiwa simba alikuwa hachezi alipoenda yanga akapata nafasi ya kucheza,Niyonzima akiwa yanga alikuwa tegemeo na  alipoenda simba kwa mda mchache aliokuwa fiti alifanya makubwa kuwatapisha mashabiki wa simba majukwaani.
    Usajili wa wawili hao kutoka kwenye vilabu vyao haukuwa wa kumreplace mwingine,ndio maana yanga walimsajili Ajib wakiwa wanajua hata Niyonzima wataendelea kuwa nae.
    Utamu wa vipaji vyao ni chachu kwa vijana wanaochipukia kwa sasa ingawa Ajibu bado hajafanikiwa kuiteka nafasi katika kikosi cha kwanza cha simba amekuwa akiingia na kutoa kwa sehemu tu kile alichojaaliwa.Bado nilitamani kuwaona wakiupiga katika kikosi kimoja tena itakuwa Simba au Yanga hapo niwaachie wazee wa kutabiri wafanye yao.

    (Dominick Salamba ni mchambuzi wa soka anapatikana kwa namba +255 713 942 770 pia kupitia katika Akaunti yake ya instagram kama @dominicksalamba)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AMBAVYO AKILI ZA NIYONZIMA TOFAUTI NA MIGUU YA AJIBU! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top