• HABARI MPYA

  Monday, January 27, 2020

  AZAM FC YAICHAPA FRIENDS RANGERS 3-1 NA KUFUNGA MLANGO WA 16 BORA KOMBE LA TFF

  Na Asha Said, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Azam FC imefunga mlango wa kuingia hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Friends Rangers ya Daraja la Kwanza jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Kwa matokeo hayo, Azam FC ambao ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo, sasa wataifuata Ihefu Jijini Mbeya kuwania tiketi ya Robo Fainali ya michuano hiyo.
  Katika mchezo wa leo, mabao ya Azam FC yamefungwa na Iddi Kipagwile mawili dakika za 43 na 53 na Said Mourad aliyejifunga dakika ya 47 ambaye pia ndiye aliyefunga bao pekee la Friends Rangers dakika ya 85.

  Azam FC inaungana na Yanga, Simba, Kitayosa, Namungo FC, Kagera Sugar, Stand United, Alliance FC, Ndanda SC, Ihefu FC, JKT Tanzania, Gwambina FC, Sahare All Stars, KMC, Panama na Mbeya City kuingia raundi ya tano ya michuano hiyo ambayo bingwa wake hucheza michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  Katika hatua hiyo, mbali na Azam kuwa wageni wa Ihefu, Simba watakuwa watakuwa wageni wa Stand United, Yanga watakuwa wenyeji wa Gwambina, Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa KMC, Ndanda wataikaribisha Kitayosa, Mbeya City wataikaribisha Namungo, JKT Tanzania wataikaribisha Alliance FC na Panama watakuwa wenyeji wa Sahare All Stars.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA FRIENDS RANGERS 3-1 NA KUFUNGA MLANGO WA 16 BORA KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top