• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 27, 2020

  MECHI MBILI HAZITOSHI, TUNAHITAJI KUMPA MUDA ZAIDI BEN MORRISON

  Na Mustafa Mtupa, DAR ES SALAAM
  NIKIWA mmoja ya watu walio kusanyika kwenye moja ya shughuli ambayo binafsi nilialikwa. Nilipewa kazi ya kusambaza chakula.kazi ambayo niliifanya kwa ufasihi kabisa.lakini nilipofika kwenye moja ya duara  lilioundwa na wazee waliokuwa bize huku sauti zao zikionekana kuwa zenye upole na zilizo hitaji usikivu wa hali ya juu ili kusikia kuwa walikuwa wanajadili nini.
  Ilionesha wazi kuwa wote walikuwa wanaunga mkono kile ambachi kilikuwa kinaongelewa kwani hakuonekana hata mmoja kati yao akionesha Haiba ya ubishi.
  Hulka yangu ya udadisi ilinifanya nilisumbue sikio langu kwa kusikiliza kwa makini sauti hizo ndogo.zilizo ashiria kubeba ujumbe mzito.

  Nilimsikia mmoja ya wazee wale akisema kuwa "Morisson ndiyo mchezaji wetu bora kwa sasa,mimi naona pale tumelamba dume kabisa"
  Ghafla nikashtuka na nikahisi kama presha ina nipanda baada ya kusikio maneno hayo.kumbu kumbu ikanipeleka kwa mwalimu wangu wa kidato cha tano ambaye siku moja aliwahi kuniimbia shairi la mmoja ya manguli wa utungaji wa mashairi hapa nchini Marehemu Shaban Robert aliwahi kuimba.
  "Halina kificho penzi liingiapo,mwenye mapenzi haoni ingawa anayo macho."
  Akilini mwangu nikagundua kuwa kinacho wasumbua wazee hawa ni Mapenzi tu.jambo ambalo linawafanya washindwe kuusemea  uhalisia.
  Ni jambo la kuukosea Heshima sana mpira wa miguu kuamini kuwa Morrison ni daraja la Kanda,Chama na okwi kwa mechi mbili ambazo amecheza .
  Kiuhalisia anahitaji majaribio zaidi ili kutufanya tuamini kwenye miguu yake.japokuwa kiwango alicho onesha katika mchezo wake wa kwanza na wapili. kilikuwa ni kiwango cha upekee sana japo haiwezi kutufanya wapenzi wa soka hapa nchini kwamba ameiweza ligi kuu.
  Siku moja wakati napita pita kwenye moja ya Magroup ya Whatsapp nilikutana na ripoti ya skauti kutoka nchini Italia. ambayo ilivuja,ripoti hii ilikuwa inaonesha maendeleo ya mchezaji Fulani kwa muda wa karibia mwaka mmoja na mchezaji huyu sio kwamba ni chipukizi,!hapana,alikuwa ni mchezaji mwandamizi kabisa lakini skauti alihitaji zaidi ya mwaka mmoja kabla ya kujiridhisha kuwa anafaa
  Kimsingi mpira una matokeo ya kikatili sana hivyo tusimtoe chambo kwani akifeli atakuwa anafeli pia kwa sababu ya kuwa tulimfanya aone ana deni kubwa la kulipa kwakuwa muliamini kuwa ndiyo mkombozi wenu.hivyo akiwa kiwanjani hatokuwa huru. zaidi atafanya vitu vingi ili kuwaaminisha kuwa yeye ni bora mwisho sehemu ya kupiga atataka apige kanzu na hapo ndipo wanayanga  wa tawi la Mbagala kiburugwa watakapo anza kumuona kama Jaja.
  Baada ya shughuli hiyo kuisha nilipita kwenyee moja ya sehemu wanazouzia magazeti na kukutana na kichwa cha habari kinachosema kuwa 'Morrison asema ana kazi ngumu ya kufanya" binafsi nilipenda mapekeo ya maneno ya mashabiki kwenye mdomo wake ila shida ni kuwa je? Mapokeo hayo ya mdomoni yanafanana na kwenye ubongo? Inawezekana ubongo wake unasadiki kuwa yeye tayari ni bora lakini hulka ya Aibu ikamfanya aseme kuwa ana kazi kubwa ya kufanya.
  Mimi naenda zangu kulala maana pilau limenilevya lakini bado naendelea kutafakari kuhusu huyu ' Morisson na maajabu ya miguu yake'

  @Mustafa.Mtupa

  0687058966
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MECHI MBILI HAZITOSHI, TUNAHITAJI KUMPA MUDA ZAIDI BEN MORRISON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top