• HABARI MPYA

    Tuesday, January 28, 2020

    DK. MSOLLA AITISHA MKUTANO WA DHARURA WA WANACHAMA YANGA FEBRUARI 16 JKNICC

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Yanga inatarajiwa kufanya mkutano wa dharula Februari 16, mwaka huu katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Kambarage Nyerere (JKNICC), Dar es Salaam kuanzia Saa 4:00 asubuhi.
    Taarifa ya Mwenyekiti wa Yanga SC, Dk. Mshindo Mbette Msolla kwa vyombo vya Habari leo imesema kwamba ameitisha mkutano huo kwa kuzingatia Ibara ya 22 ya Katiba ya mwaka 2010.
    Msolla amesema mkutano huo utakuwa na ajenda sita ambazo ni; Ufunguzi wa Mkutano, Kuthibitisha Akidi ya Mkutano, Kupitia Ajenda za Mkutano, Kuwasilisha na Kuainisha Mapendekezo ya Katiba/Mapendekezo Mapya, Kupigia Kura Mapendekezo ya Marekebisho ya Katiba na Kufunga Mkutano.
    Msolla, aliyewahi kuwa kocha Mkuu wa Taifa Stars, aliingia madarakani Yanga  Mei 5, mwaka jana katika uchaguzi uliofanyika leo Bwalo la Maofisa wa Jeshi la Polisi, Osyterbay mjini Dar es Salaam akishinda kwa kishindo dhidi ya Dk. Jonas Benedict Tiboroha.
    Msolla alipata jumla ya 1,276 dhidi ya 60 tu za Daktari mwenzake, Tiboroha aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo chini ya uongozi uliopita.
    Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilikwenda kwa Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Mwakalebela aliyepata kura 1,206 akiwashinda Janneth Mbene (Mbunge)aliyepata kura 61, Titus Osoro kura 17, Yono Kevela kura 31 na Chota Chota kura 12.
    Na walioshinda nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Hamad Islam aliyepata 1,206, Mhandisi Bahati Faison Mwaseba kura 1,174, Dominick Ikute kura 1,088, Kamugisha Kalokola kura 1,072, Arafat Haji kura 1,024, Salum Ruvila kura 976, Saad Khimji kura 788 na Rodgers Gumbo kura 776. 
    Uchaguzi huo ulifuatia kujiuzulu kwa viongozi wote waliongia madarakani Juni 11 mwaka 2016, Mwenyekiti Yussuf Manji, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na wajumbe wao, Siza Augustino Lymo, Tobias Lingalangala, Samuel Lukumay, Hussein Nyika, Omary Said Amir, Salum Mkemi, Ayoub Nyenzi na Inspekta Hashim Abdallah.
    Pamoja na kuwa kocha wa Taifa Stars, Dk. Msolla pia amewahi kuwa mtumishi wa Serikali kwa nafasi mbalimbali, ikiwemo Ukurugenzi wa Uendelezaji wa Mazao katika Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika wakati wa awamu ya Nne chini ya Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DK. MSOLLA AITISHA MKUTANO WA DHARURA WA WANACHAMA YANGA FEBRUARI 16 JKNICC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top