• HABARI MPYA

    Wednesday, January 29, 2020

    MCHEZAJI KUPELEKWA KWA MKOPO NI UAMUZI WA BENCHI LA UFUNDI

    Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM
    DIRISHA dogo la usajili msimu huu limetuletea taswira ya kushangaza sana kwa wachezaji wetu na waajiri wao.
    Kuna kitu kinaitwa usajili wa mkopo,hii inamaanisha kuwa,klabu X inaweza kumtumia mchezaji ambae anamilikiwa na klabu nyingine na wao kumtumia kwa makubaliano maalum kutoka timu x,mchezaji husika na timu inayohitaji huduma ya mchezaji husika.
    Kwa nini usajili wa mkopo? kabla ya kulijua hilo kila mmoja anapaswa kujua kuwa kila timu inasajili wachezaji kwa ajili ya kuwatumia katika mashindano tofauti ndani ya msimu,kisha tufahamu kuwa uamuzi wa kumpeleka mchezaji kwa mkopo mahali fulani ni uamuzi wa benchi la ufundi,baada ya kutathmini nafasi ya mchezaji huyo kwenye timu, hapo ndipo utagundua kuwa mchezaji anaweza kupelekwa kwa mkopo ili kulinda kipaji chake,na ni kwa faida ya timu husika endapo mchezaji ataimarika kwa siku zijazo..
    👉🏽👉🏽Katika nchi za wenzetu zilizopiga hatua kisoka mara nyingi wachezaji wanaopelekwa kwa mkopo ni wale vijana wadogo ambao wanakwenda kupata uzoefu na nafasi ya kucheza ila waje kuwa na manufaa katika siku zijazo.
    Ingawa kuna wakati hata wachezaji wazoefu utolewa kwa mkopo huku kukiwa na kipengele cha mauziano ya jumla baada ya muda fulani jambo ambalo limekuwa lina tija kwa pande zote tatu kwa maana ya Mchezaji husika,timu yake anayotoka na ile timu anayokwenda.
    Ndio mana hata David Beckham,Kurt Zouma,Michy Batshuayi na wengine wengi walipotolewa kwa mkopo hakukuwa na kelele wala malalamiko kila upande ulitulia kwani faida zilikuwa za pande zote kwa maana kuna mnufaika wa sasa na baadae lilikuwa ni swala la kila mmoja kufurahi kwa wakati wake kwa kadri ya makubaliano yao.
    😊😊Mkataba wa mkopo unatakiwa  kuwa na vipengele vitakavyomlinda na kumsaidia mchezaji  ili aweze  kuimarika zaidi.
    Mfano kipengele cha kumfanya mchezaji apewe nafasi kwenye kikosi cha kwanza,kuboreshewa maslahi yake haya yote yanalengwa kuangalia mustakabali wa baadae wa mchezaji.
    Lakini kipengele cha kumzuia mchezaji asicheze mechi baina na timu yake ya zamani ikiwa lengo kuilinda klabu yake hiyo kimatokeo.
    Pia kupunguza mshahara au kusaidiana katika kumlipa mchezaji baina ya pande mbili,hizo zote ni namna za kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.👏🏽👏🏽👏🏽
    Pamoja na yote mkopo wa mchezaji  wakati mwingine huzingatia mahusiano baina ya timu hizo ndio mana unakuta timu mbalimbali zinaingia ushirika wenye manufaa kwa pande zote mbili kwa kuzingatia mahitaji na matamanio ya kila upande wazungu wanasema win-win situation.
    Tatizo la soka letu ni namna ambavyo timu zetu zinaseti malengo yake inakuwa ngumu kujua ni malengo ya muda mfupi au mrefu,unakwenda mbali zaidi nani anasajili,na anasajili kwa matakwa ya timu au mfuko wake kadri alivyojaaliwa,je benchi la ufundi lina huitaji na huyo mchezaji au ni mihemko tu ili kufurahisha mashabik..
    Kutokana na hayo ndipo matatizo yanapo anza sio ajabu katika soka letu mchezaji kasajiliwa julai ikifika januari anaonekana hafai na kipindi chote alichosajili hajatumika na anatakiwa aachwe dirisha dogo au apelekwe kwa mkopo kwa kuhofia kuvunja mkataba jambo ambalo litaigharimu klabu sasa unajiuliza alisajiliwa ili iwe nini na aliye msajili ndiye aliyetaka kumtumia au alisajili mwingine kwa matumizi ya mtu mwingine? aisee kizunguzungu.
    Hivi umewahi kujiuliza wachezaji wangapi katika soka letu walitolewa kwa mkopo na baadae wakarudi wakiwa wameiva katika vilabu vyao na kunufaika na mkopo husika? kama jibu ni hapana ndio mana huwezi kushangaa kusikia wachezaji wanagoma kwenda kwa mkopo katika vilabu vingine kwani wanajua ni sawa na kujitumbukiza baharini.
    Narudia tena mchezaji kwenda timu fulani kwa mkopo huo ni uamuzi wa benchi la ufundi katika harakati za kulinda kipaji chake, si sawa mchezaji kugoma kwenda mahala fulani kwa mkopo,ni sehemu ya mkataba wake.
    Kuna haja ya vilabu vyetu kuboresha namna ya kufanya usajili,vinginevyo inaleta shida na migogoro isiyo na ulazima katika soka la kisasa ndio mana unakuta kila dirisha timu inasajili zaidi ya wachezaji 10 jambo ambalo sio sawa na alileti afya katika ustawi wa mpira wetu.
    Usajili sio swala la kukurupuka mchezaji amewafunga katika mechi saa 10 jioni usiku saa 2 mnamsajili asubuhi anatangazwa hapana..Lazima ufanyike upembuzi wa kina kuwe na timu makini za kuskauti wachezaji katika maeneo mbalimbali na klabu inapata taarifa sahihi na kwa kutumia benchi la ufundi ndipo usajili unafanyika..
    Kwa upande mwingine wachezaji wetu badilikeni ufike wakati mkubali kuwa chini ya mawakala makini ambao watawasidia katika mambo ya kutafsiri na kuwashauri nini cha kufanya katika safari yenu ya maisha ya soka, sio unamchukua mjomba,kaka ambaye hana weledi katika maswala ya soka mwishoe mnaingia matatizoni na kupoteza mwelekeo..
    Wakati timu inakuitaji ndio wakati wa kuweka mambo sawa na kulinganisha mkataba wa klabu na mahitaji yako ndio mana hata dili la Samatta lilichelewa ni kwa sababu ya upande wa Samatta na upande wa Aston villa walikuwa wakijaribu ya kuhakikisha kila upande unapata kinachostahili na kilichobora..Sio unatakiwa asubuhi jioni tayari upo mezani umetoa meno yote umeshikishwa peni upande wa juu maandishi yanasomeka DEAL DONE.😂😂😂😂
    Mwisho chama cha wachezaji SPUTANZA mnawajibika kuendelea kutoa elimu na ufahamu zaidi kwa wachezaji wetu kwa kushirikiana na mamlaka ya Soka letu TFF pamoja na serikali kupitia Baraza la Michezo Tanzania BMT katika kuendeleza soka letu na hali za wachezaji wetu.

    (Dominick Salamba ni mchambuzi wa soka anapatikana pia kupitia katika Akaunti zake za: instagram@dominicksalamba  Twitter:@dominicksalamb1 au simu namba +255 713 942 770)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MCHEZAJI KUPELEKWA KWA MKOPO NI UAMUZI WA BENCHI LA UFUNDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top