• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 22, 2020

  STARS YAPANGWA NA DRC, BENIN NA MADAGASCAR KUWANIA TIKETI YA KOMBE LA DUNA 2022 QATAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TANZANIA imepangwa Kundi J katika kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Benin na Madagascar.
  Katika droo iliyopangwa jana Jijini Cairo, Misri ikihusisha nchi 40 wanachama wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) jumla ya makundi yalipangwa katika hatua hii ya pili ya mbio za Qatar 2022.
  Kundi A linaundwa na mabingwa wa Afrika, Algeria, Burkina Faso, Niger na Djibouti, Kundi B Tunisia, Zambia, Mauritania na Equatorial Guinea, Kundi C Nigeria, Cape Verde, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) na Liberia.

  Kundi D linazikutanisha Cameroon, Ivory Coast, Msumbiji na Malawi, Kundi E Mali, Uganda, Kenya na Rwanda, Kundi F Misri, Gabon, Libya na Angola, Kundi G Ghana, Afrika Kusini, Zimbabwe na Ethiopia, Kundi H Senegal, Kongo, Namibia na Togo na Kundi I Morocco, Guinea, Guinea-Bissau na Sudan.
  Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa mwenye asili ya Ghana, Marcel Desailly na kocha wa timu ya taifa ya wanawake ya Ivory Coast, Clementine Toure ndyo waliomsiadia Mkurugenzi wa Mashindano wa CAF, Samson Adamu kupanga makundi hayo, ambayo mechi zake za kufuzu zitaanza Oktoba 2020 hadi Oktoba 2021
  Baada ya timu zote kucheza nyumbani na ugenini, washindi wa makundi yote 10 watafuzu kwa hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tketi ya Qatar.
  Katika hatua ya mwisho timu hizo 10 zitamenyana baina yao na washindi watano ndiyo watapewa tiketi za kuiwakilisha Afrika kwenye fainali za Kombe la Dunia zinazotarajiwa kuanza Novemba 21 hadi Desemba 18 mwaka 2022 nchini Qatar.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: STARS YAPANGWA NA DRC, BENIN NA MADAGASCAR KUWANIA TIKETI YA KOMBE LA DUNA 2022 QATAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top