• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 31, 2020

  AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA MTIBWA SUGAR TAIFA TIMU ZOTE ZIKIMALIZA PUNGUFU

  Kiungo wa Mtibwa Sugar, Salum Kihimbwa akiupitia mpira mguuni mwa beki Mganda wa Azam FC, Nicholas Wadada katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Alhamisi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Timu hizo zilitoka sare ya 1-1, Mtibwa Sugar wakitangulia kwa bao la Ismail Mhesa dakika ya 67, kabla ya Muivory Coast, Richard Ella D'jodi kuisawazishia Azam FC kwa penalti dakika ya 77. 
  Timu zote zilimaliza pungufu baada ya wachezaji wake kuonyeshwa kadi za pili za njano na kutolewa kwa kadi nyekundu, wakianza Mtibwa Sugar waliompoteza beki wao, Dickson Job dakika ya 72 kabla ya mshmabuliaji wa Azam, Shaaban Chilunda kutolewa dakika ya mwisho kabisa, 90 na ushei. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA MTIBWA SUGAR TAIFA TIMU ZOTE ZIKIMALIZA PUNGUFU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top