• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 16, 2020

  JUVE, MILAN, INTER ZALITOLEA MACHO TAJI LA COPPA ITALIA

  LICHA ya Michuano ya Coppa Italia kufikia  hatua ya 16 bora,Vilabu vikubwa nchini humo kama Juventus ,Ac Milan,Lazio  na Inter vyenyewe vimeanza rasmi safari ya kuwania taji hili wiki hii.
  Utaratibu wa Coppa italia ni kuwa vilabu nane vya juu katika msimamo uliopita wa Serie A hupata tiketi ya kuanzia katika hatua ya 16 bora yaani baada ya washindi wa Raundi ya nne kupatikana katika msimu unaofuatia.
  Wakiwa na Kumbukumbu ya kutwaa Coppa Italia mara nne mfululizo kabla ya kulipoteza msimu uliopita Kwa Lazio, Juventus wakiongozwa na Paulo Dybala walianza vema safari ya Coppa Italia 2019/20  baada ya kuwachapa Udinese kwa mabao 4-0 usiku wa tar 15 January.
  Usiku wa leo Tar 16 January, AS Roma watakuwa ugenini kukipiga na Parma. Uwepo wa nyota Gervinho kwa upande wa Parma unaufanya mchezo huu kuwa na mtazamo wa tofauti kidogo katika kufikiria juu ya matokeo baada ya Dakika 90. AS ROMA haijawa bora sana msimu huu wa Serie A ,ila hili haliwatoi wao katika listi ya moja ya vilabu vinavyopewa nafasi kubwa kutwaa Coppa Italia msimu huu.Uwepo wa Nyota kama Edin Dzeko,Pellegrini na beki mzoefu Chris Smalling unaipa Roma hatua moja mbele ya Parma katika mechi hii hasa juu ya ukubwa wa kikosi.
  Majeraha mabaya ya Goti alioyapata nyota wao Nico Zaniolo ndio taarifa mbaya zaidi kwa Roma kuelekea mchezo huu. Majeraha ya Zaniolo yanatoa nafasi kwa nyota wengine kuonyesha ubora wao ndani ya Roma.
  Ushindi katika mchezo huu utaifanya timu mojawapo baina ya Parma na AS Roma kuwavaa Juventus katika mchezo wa Robo fainali ya  michuano hii.
  Inter Milan ni moja ya timu zinazopewa nafasi kubwa msimu huu katika mashindano ya soka la Italia ,ikichagizwa na uwepo wa kocha mpya Antonio Conte na Straika mbelhiji Romelu Lukaku waliibugiza Cagliari kwa mabao 4-1 katika dimba la Giuseppe Meazza huku Lukaku akirudi kambani mara mbili na kutimiza mabao 18 tangu msimu huu uanze. Inter wakawa wamefanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali.
  @startimestz inaonesha LIVE michuano hii na Safari imeanzia katika Roundi ya 16 bora na itaishia katika fainali ya michuano hii .Usipitwe,j iunge na @startimestz Sasa.
  #StartimesON
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: JUVE, MILAN, INTER ZALITOLEA MACHO TAJI LA COPPA ITALIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top