• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 23, 2020

  CHIPUKIZI WA AZAM FC AKADEMI ATUA UFARANSA KUJIUNGA NA KLABU YA FC NANTES

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  NYOTA wa timu ya vijana ya Azam FC 'Azam U-20' na timu ya Taifa ya Vijana 'Ngorongoro Heroes', Tepsi Evance, amewasili nchini Ufaransa kwa ajili ya kujiunga na timu ya Nantes.
  Tepsi aliondoka jana pamoja na wakala anayetambulika na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Kambi Seif kwenda Nantes kwa ajili ya mafunzo hadi atakapotimiza umri wa miaka 18 baadae mwaka huu asaini mkataba.
  Evance atakapofikisha umri huo, atajiunga moja kwa moja na timu ya wakubwa ya Nantes inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo (Ligue 1). 

  Tepsi Evance akiwa makao makuu ya klabu ya Nantes baada ya kuwasili Ufaransa jana

  Tepsi ni mmoja kati ya vijana wanne waliopatikana kwenye usahili uliofanywa na Cambiasso Sports na Rainbow Sports Novemba mwaka jana, kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Mchezaji mwingine wa Azam U-20, aliyefuzu kwenye usahili huo ni nahodha, Samuel Onditi, ambaye anasubiria taratibu za Visa zikamilike sambamba na wachezaji wengine wawili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHIPUKIZI WA AZAM FC AKADEMI ATUA UFARANSA KUJIUNGA NA KLABU YA FC NANTES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top