• HABARI MPYA

    Monday, January 20, 2020

    KAMA SIYO UZIWANDA, SAMAGOL ANGEKUWA WA PILI ASTON VILLA

    Na Ibrahim Mkemia, DAR ES SALAAM
    KAMA ningekuwa mtu wa takwimu kwa sasa ningesema kuwa "asilimia 99.9% ya watanzania ndio wanaongoza kwa kuperuzi mitandao ya kijamii. Hasa kwenye mtandao maarufu wa Instagram na mitandao mengine ambayo ni vyanzo vya taarifa za michezo duniani.
    Hii imekuja baada ya kupata taarifa kuwa mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya genk ya ubelgiji. Kuwa anatakiwa na klabu inayoshiriki ligi kuu uingereza ambayo ni Aston villa. Mbwana ally samatta kwa sasa ndo jina ambalo limekuwa midomoni mwa watanzania wengi sana ndani ata nje ya nchi.
    Imekuwa kama ndoto kwa watanzania wengi baada ya kusikia kuwa nahodha wao kutakiwa na klabu inayoshiriki ligi pendwa duniani kwa maana ya (English premier league) na imekuwa matamanio ya watu wengi kwani ndo mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kucheza kwenye ligi hiyo kubwa na bora zaidi ikiwa kwenye ligi tano bora.
    Wakati stori za samatta zikiendelea kushika kasi na kuenea kwenye baadhi ya mitandao maarufu duniani. Nakutana mzee mmoja maeneo ya daraja la Nyerere kigamboni akitambulika kama Mr kalomo akaniambia "kama Mohammed kaburu mama ake angekubali basi huyu samatta ata asingeimbwa hivi" Nikamuuliza Mohammed kaburu?  Akajibu ndio akaniweka chini na kuanza kunipa darasa kuhusu huyo Mohammed kaburu.
    Mnamo mwaka 1973 timu ya Aston villa ilikuja kufanya ziara ya kimichezo nchini Tanzania na ilifanikiwa kucheza na timu ya yanga, simba, na Zanzibar combine. Wakati wanacheza na yanga kocha wa Aston villa aliona kiwango cha Mohammed kaburu ambaye alikuwa chini ya kocha wa yanga aliyekuwa anaitwa Tambwelea.  Yanga walimpata Mohammed kaburu walipoenda kufanya ziara yao mjini Lindi. Na huko walifanikiwa kuondoka na wachezaji watatu akiwemo mwenyewe Mohammed kaburu, Matokeo pamoja na Muhaji muki. Yanga walienda huko baada ya kuchukua ubingwa wa Tanzania bara. Na ilikuwa kama tabia kwa timu kubwa kufanya ivyo kwenda kwenye baadhi ya mikoa kutembeza kombe lao.
    Mohammed kaburu alikuwa ni mtoto pekee kwenye familia yao na ilikuwa ngumu kwa mama ake kuweza kumruhusu mwanae kuondoka na wazungu na ikizingatia kipindi iko mambo ya mitandao kulikuwa amna ivyo "mama kaburu" alijua mwanae anaenda sehemu ambayo si salama kwake. Katika mechi dhidi ya Aston villa Mohammed kaburu alicheza kwa kiwango kikubwa sana. Kwa lugha ya mtaani wanasema "aliupiga mwingi mno" na ikawalazimu viongozi wa Aston villa pamoja na kocha wao Ron Sounder kushawishika kutaka kuondoka nae.
    Ila waswahili wanasema "kisicho riziki hakiliki" na hii ndo ikawa kauli ya Mohammed kaburu kwa wakati huo.  Ila kama wazazi wangekubali basi mbwana ally samatta angekuwa mchezaji wa pili kucheza kwenye klabu ya astoni villa.  
    Ambayo kipindi iko ilikuwa inashiriki ligi daraja la kwanza (FIRST DIVISION) ambayo kwa sasa ivi ndo ligi kuu ya uingereza.
    Jina la "kaburu" lilitokana na Mohammed kaburu kuwa na rangi ang'avu kidogo na kwa wakati huo watu wa aina hiyo walitaniwa kwa kuitwa jina hilo. Wakifananishwa na wazungu ambao waliishi kusini mwa Africa  (south Africa) na Mohammed akaitwa ivyo na likawa jina maarufu sana.
    Kwa sasa mzee Mohammed kaburu anaishi kigamboni na maisha yanaendelea. Ila ndugu yangu mbwana ally samatta sehemu unayoenda ni sahihi kwako na ujisikie uko nyumbani kwa sababu Aston villa ni ndugu zetu kabisa bila kupepesa macho. Nakutakia mafanikio yenye faida. @samagol77
    ✒imeandikwa na @mkemia_tza
    →kalomoibrahim@gmail. com
    →0715147449
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAMA SIYO UZIWANDA, SAMAGOL ANGEKUWA WA PILI ASTON VILLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top