// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HOMA YA MECHI YA NGAO, YANGA HAOOOO MBEYA, AZAM FC WAFUATA ‘KARAFUU’ ZENJI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HOMA YA MECHI YA NGAO, YANGA HAOOOO MBEYA, AZAM FC WAFUATA ‘KARAFUU’ ZENJI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, August 07, 2015

    HOMA YA MECHI YA NGAO, YANGA HAOOOO MBEYA, AZAM FC WAFUATA ‘KARAFUU’ ZENJI

    Na Mwandishi Wettu, DAR ES SALAAM
    WAKATI Yanga SC wanatarajiwa kuondoka kesho kwenda Mbeya kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii, wapinzani wao, Azam FC nao watakwenda visiwani Zanzibar.
    Azam FC ambao Jumapili iliyopita walitwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame wametua Zanzibar leo kwa kambi ya wiki mbili.
    Azam FC iliifunga mabao 2-0 Gor Mahia ya Kenya katika fainali ya Kagame Jumapili, ikitoka kushinda 1-0 dhidi ya KCCA ya Uganda katika Nusu Fainali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Azam FC na Yanga SC zilimaliza dakika 90 bila kufungana kabla ya mshindi kupatiaka kwa mikwaju ya penalti Jumatano iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

    Azam FC na Yanga SC watamenyana Jumamosi ya Agosti 22, mwaka huu katika mchezo wa Ngao, kuashiria upenuzi wa pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itakayofuatia katikati ya Septemba.
    Kikosi kizima cha Azam FC jana kilikuwa Ikulu, Dar es Salaam kwa mwaliko wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kupeleka Kombe la Kagame.
    Na Rais Kikwete alifurahia timu hiyo kubakiza taji nyumbani ikishinda mechi zote, tena bila ya kuruhusu nyavu zao kuguswa.
    Mechi ya Agosti 22 inatarajiwa kuwa ya kukata na shoka kutokana na upinzani wa Azam FC na Yanga SC katika miaka ya karibuni, zikiwa ndizo timu ambazo zinapokezana ubingwa wa Ligi.
    Na ikumbukwe mara ya mwisho zilipokutana wiki iliyopita katika Robo Fainali ya Kombe la Kagame timu hizo zilimaliza dakika 90 bila kufungana kabla ya Azam FC kushinda kwa penalti 5-3.
    Maana yake, mechi Agosti 22 ni marudio ya mchezo wa Kombe la Kagame.
    Kama ilivyokuwa katika Kagame, kwenye mechi ya Ngao pia, iwapo timu hizo hazitafungana ndani ya dakika 90, sharia ya mikwaju ya penalti itaamua mshindi. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HOMA YA MECHI YA NGAO, YANGA HAOOOO MBEYA, AZAM FC WAFUATA ‘KARAFUU’ ZENJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top