• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 22, 2015

  HASIRA ZA MAN UNITED KUMKOSA PEDRO, VAN GAAL ASEMA; "DE GEA HAUZWI NG'O"

  KOCHA Louis van Gaal amesema kipa David De Gea hataondoka Manchester United kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
  De Gea anakuwa jukwaani kwa mara nyingine wakati United inamenyana na Newcastle Uwanja wa Old Trafford muda huu, kwa sababu Van Gaal anafikiri Mspanyola bado akili yake haijatulia akifikiria uhamisho wa Real Madrid.
  Kwa mujibu wa ripoti nchini Hispania, mabingwa mara 10 wa Ulaya watatoa ofa ya kumnunua kipa huyo kabla ya dirisha la usajili kufungwa Septemba 1, mwaka huu.
  Klabu ya Real Madrid inamtaka David de Gea kabla ya dirisha la usajili kufungwa

  Lakini baada ya United kumkoa Pedro aliyehamia Chelsea wiki hii kutoka Barcelona, Van Gaal 'amewaka' katika Mkutano na Waandishi wa Habari jana.
  "Nafikiri Manchester United inapotaka mchezaji, atakuja, tofauti na klabu inapoamua haiuzi mchezaji," amesema kocha huyo United. "Ni saw na kwetu, hatumuuzi De Gea,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HASIRA ZA MAN UNITED KUMKOSA PEDRO, VAN GAAL ASEMA; "DE GEA HAUZWI NG'O" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top